Halloween Costume ideas 2015
Latest Post

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : HYPERLINK "http://www.ikulu.go.tz"www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu katika Wizara mbalimbali.
Walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi - Ombeni Sefue
Katibu Mkuu Ikulu
Peter Ilomo
Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
Dkt. Laurian Ndumbaro
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu)
Dkt. Deo Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu - Afya)
Bernard Makali (Naibu Katibu Mkuu - Elimu)
Ofisi ya Makamu wa Rais
Mbaraka A. Wakili ( Katibu Mkuu)
Mhandisi Ngosi Mwihava (Naibu Katibu Mkuu)

Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu)
Erick Shitindi (Katibu Mkuu Kazi na Ajira)
Mussa Uledi (Katibu Mkuu Bunge)
Dkt. Hamis Mwinyimvua (Katibu Mkuu - Sera)
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Dkt. Frolence Turuka (Katibu Mkuu - Kilimo)
Dkt. Mashingo (Katibu Mkuu Mifugo)
Dkt. Budeba (Katibu Mkuu - Uvuvi)

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Joseph. Nyamuhanga (Katibu Mkuu - Ujenzi)
Dkt. Leonard M. Chamuliho (Katibu Mkuu - Uchukuzi)
Profesa Faustine R. Kamuzora (Katibu Mkuu - Mawasiliano)
Mary Sassabo (Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano)
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Dkt. Yamungu Kayandabira (Katibu Mkuu)
Dkt. Moses Kusiluka (Naibu Katibu Mkuu)
Wizara ya Maliasili na Utalii
Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi (Katibu Mkuu)
Anjelina Madete (Naibu Katibu Mkuu)
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Dkt. Adelhem James Meru (Katibu Mkuu - Viwanda)
Profesa Adolf F. Mkenda (Katibu Mkuu - Biashara na Uwekezaji)
Mhandisi Joel Malongo (Naibu Katibu Mkuu)

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
Maimuna Tarishi (Katibu Mkuu)
Profesa Simon S. Msanjila (Naibu Katibu Mkuu)
Dkt. Leonard Akwilapo (Naibu Katibu Mkuu)
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya (Katibu Mkuu - Afya)
Sihaba Nkinga (Katibu Mkuu - Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto)
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Profesa Elisante Ole Gabriel Mollel (Katibu Mkuu)
Nuru Halfan Mrisho (Naibu Katibu Mkuu)
Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Mhandisi Mbogo Futakamba (Katibu Mkuu)
Mhandisi Kalobero Emmanuel (Naibu Katibu Mkuu)
Wizara ya Nishati na Madini
Profesa Justus W. Ntalikwa (Katibu Mkuu)
Profesa James Epifani Mdoe (Naibu Katibu Mkuu)
Dkt. Paulina Pallangyo (Naibu Katibu Mkuu)
Wizara ya Katiba na Sheria
Profesa Sifuni Mchome (Katibu Mkuu)
Suzan Paul Mlawi (Naibu Katibu Mkuu)
Amon Mpanju (Naibu Katibu Mkuu)
Wizara ya Mambo ya Ndani
Jaji Meja Jenerali Projest A. Rwegasira (Katibu Mkuu)
Balozi Hassan Simba Yahaya (Naibu Katibu Mkuu)

Wizara ya Fedha na Mipango
Dkt. Silvacius Likwelile (Katibu Mkuu)
Dorothy Mwanyika (Naibu Katibu Mkuu)
James Dotto (Naibu Katibu Mkuu)
Amina Hamis Shaban (Naibu Katibu Mkuu)
Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Dkt. Aziz Mlima (Katibu Mkuu)
Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi ( Naibu Katibu Mkuu)
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Job D. Masima (Katibu Mkuu)
Immaculate Peter Ngwale (Naibu Katibu Mkuu

Makatibu wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wote ambao hawajatajwa katika orodha hii watapangiwa kazi nyingine.
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Eliakimu Maswi kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na ametengua uteuzi wa Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Lusekelo Mwaseba, ambaye atapangiwa kazi nyingine

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
30 Desemba, 2015


 

                   

Je unakumbuka Hali ya hewa ya El Nino iliyowahi kutokea na kusababisha maafa makubwa katika nchi za Afrika ikiwemo Tanzania na Kenya. Mvua kubwa iliyobatizwa jina la El Nino kutokana na hali ya hewa hiyo iliikumba Tanzania na Kenya kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati na kusababisha maafa makubwa huku ikiwaacha wananchi bila makazi baada ya nyumba zao kusombwa na Mafuriko makubwa ya maji yaliyotokana na mvua hiyo....,




Hali ya hewa ya El Nino ambayo imekuwa ndiyo kali zaidi katika historia itazidisha hatari ya njaa na maradhi kwa mamilioni ya watu duniani 2016, mashirika ya misaada yamesema.

Hali hii ya hewa inatarajiwa kusababisha ukame baadhi ya maeneo na mafuriko kwingine.
Baadhi ya maeneo yanayotarajiwa kuathirika sana yako Afrika, huku uhaba wa chakula ukitarajiwa kufikia kilele Februari.

Maeneo mengine yakiwemo Caribbea, Amerika ya Kati na Amerika Kusini yataathiriwa katika kipindi cha miezi sita ijayo.

Hali ya hewa ya El Nino, hutokana na kuongezeka kwa joto na huathiri hali ya hewa maeneo mengi. Mwaka huu hali hii imezidi na kuufanya mwaka 2015 kuwa mwaka wenye joto zaidi duniani katika historia.
Kufikia sasa, watu 31 milioni wanakabiliwa na uhaba wa chakula Afrika, theluthi moja kati ya hawa wakiwa Ethiopia.
Inakadiriwa kwamba watu 10.2 milioni watahitaji chakua cha msaada mwaka 2016.

"Tukikosa kuchukua hatua sasa, tutahatarisha zaidi maisha ya watu wasio na uwezo maeneo mbalimbali duniani,” waziri wa ustawi wa kimataifa Uingereza Nick Hurd amesema kupitia taarifa.




IRAN
                          

Iran ilizua taharuki miongoni mwa wanajeshi wa Marekani ilipofytua makombora yake karibu na meli za kubeba mizigo na manuari za kivita ya Marekani katika bahari ya Hormuz....,



 

Majaribio hayo ya makombora yake yanatarajiwa kuibua vuta ni kuvute baina ya mataifa hayo mawili miezi michache tu baada ya kutia saini makubaliano ya kinyuklia.

Iran ilifyatua makombora kadhaa takriban kilomita moja tu kutoka kwa manuari 2 za kijeshi za Marekani na Ufaransa msemaji wa jeshi la Marekani Kyle Raines alisema.
''Makombora hayo yalizua taharuki kubwa kwa majeshi yetu yaliyokuwa huko' aliongezea kusema bwana Raines.

Bahari ya Hormuz ni eneo kati ya Iran na Oman inayotumika na takriban thuluthi moja meli zinazofanikisha biashara ya mafuta kote duniani.


Hormuz ni njia muhimu inayotumika na manuari za kijeshi zinazotekeleza mashambulizi dhidi ya kundi la Islamic State.

Mwaka wa 2012 Iran ilitishia kufunga kiunganishi hicho muhimu cha mkono wa bahari yenye upana wa takriban kilomita 33.

Serikali ya Iran haijajibu shtuma hizo wala vyombo vya habari nchini humo havijaripotti kisa hicho.
Hata hivyo majeshi ya Iran yalitoa ilani ya dakika 23 pekee ya kufyatua makombora yake.

 Manuari hiyo ya kijeshi ya Marekani ni sehemu ya kikosi cha wanamaji cha 5ft Fleet kinachokita kambi katika bahari ya Bahrain.

Iran ilitia sahihi mkataba wa kutoendeleza jitihada zake za kitonaradi na imekubali kuvunjilia mbali mpango wake wa nyuklia iliiruhusiwe kuuza mafuta yake katika soko la dunia mbali na kuondolewa vikwazo dhidi yake.

Bahari ya Hormuz ndio iliyokuwa uwanja wa vita baina ya Iran na Marekani mwaka wa 1988.
Wkati huo Marekani iliharibu Manuari 6 za kijeshi za Iran mbali na kuharibu mitambo yake ya kuchimba mafuta baharini.

Mwaka wa 1988, manuari ya kijeshi ya Marekani USS Vincennes iliyokuwa katika bahari hiyo hiyo ya Hormuz iliilipua ndege ya abiria ya Iran iliyokuwa ikielekea Dubai na kuwaua abiria wote 290




MAREKANI
                    

Wendesha mashitaka katika jimbo la Pennsylvania Marekani wamemfungulia mashtaka ya kwanza mcheshi nguli Bill Cosby .

 

Cosby ameshtakiwa kwa makosa ya dhulma za kimapenzi dhidi ya mfanyikazi mmoja wa chuo kikuu kimoja nchini Marekani...,

 




Cosby alitenda kosa hilo mwaka 2004 amekana madai yeyote dhidi yake na hata amewafunguliwa mashtaka wanawake anaodai wanalenga kumpunja pesa. Awali mchekeshaji huyo alikana kufanya nao mapenzi bila ridhaa  akijitetea kuwa aliwahi kushiriki mapenzi baada ya kukubaliana na wanawake hao.

Mashtaka dhidi yake yalifufuliwa baada ya idadi kubwa ya wanawake kuibuka wakidai walipewa dawa na kisha kudhulumiwa kimapenzi na mchekeshaji huyo nguli.


Bi. Andrea Constand, aliyekuwa mfanyikazi wa chuo kikuu cha Temple ndiye aliyemshtaki Cosby mara ya kwanza mwaka wa 2005.   


https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=4415757963585234877#editor/target=post;postID=1678246762061345765

Uchunguzi ulibaini kuwa bwana Cosby alikuwa akiwapa wahasiriwa dawa aina ya Quaaludes inawalegeza na hata wengine wanasinzia kabla ya kushiriki mapenzi nao. Cosby amekiri kutumia dawa hizo za Quaaludes.

 https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=4415757963585234877#editor/target=post;postID=6084141961500910052

BURUNDI
                    


Rais wa Burundi ametishia kupigana na kikosi cha Muungano wa Afrika cha kulinda amani pindi wanajeshi hao watakapoingia nchini humo.



Akihutubia taifa kwa njia ya radio, rais Pierre Nkurunziza amesema kuingia kwa wanajeshi hao nchini Burundi kutakuwa ukiukaji wa uhuru wa taifa hilo na pia shambulizi dhidi ya serikali yake.
Rais huyo alisusia ufunguzi wa mazungumzo ya amani nchini Uganda siku ya Jumatatu.

Nkurunzinza aliyeshinda muhula wa tatu katika uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata na maasi mwezi julai mwaka huu anakana kuwepo kwa visa vya mauaji nchini mwake.

 ongozi wa kidini kutoka kanda ya Afrika Mashariki Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda ambao wamekuwa wakikutana mjini Nairobi ,wameelezea wasiwasi wao na jinsi usalama unavyozidi kudorora katika taifa hilo.

Archbishop wa Gulu, John Baptist Odama, ameiambia BBC kuwa wameiomba serikali ya Burundi kupatia mazungumzo ya amani fursa ya kuwapatanisha mahasimu nchini humo.
John Baptist Odama alisema ''Tunaisihi serikali ichukue hatua za kukomesha mauaji ya kiholela nchini humo.   Tafadhali tunawataka wakomesha mauaji zaidi ya watu  

Njia bora ya kusuluhisha mtafaruku huu ni kwa serikali na upinzani kujadiliana. Mazungumzo ya amani labda ndio suluhisho la kudumu la pekee la mzozo huu.'' alisema Odama.

Umoja wa Mataifa unakadiria watu 400 wameuawa tangu machafuko kuzuka mwezi Aprili Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kwamba angewania urais kwa muhula wa tatu.

AU  huenda ikalazimika kutuma walinda amani bila kupewa idhini na taifa mwenyeji, muungano huo utatumia kwa mara ya kwanza kifungu kwenye mkataba wake, kinachouruhusu kuingilia kati katika mataifa mengine nyakati za hatari kubwa.

Baadhi ya mambo ambayo muungano huo unaruhusiwa kuingilia kati kuzuia ni uhalifu wa kivita, mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu.
Maafisa wa UN wameonya kuwa nchi hiyo inakabiliwa na hatari ya kutumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mauaji mabaya zaidi yalitokea Ijumaa wiki iliyopita wapiganaji waliposhambulia maeneo ya jeshi Bujumbura.
Jeshi lilisema watu 87 waliuawa.
AU hata hivyo bado itahitaji kupewa idhini na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kati.





UINGEREZA
             
Kuweka akiba ni bora lakini maisha, kazi na dawa. Na ndicho ameonyesha mshambuliaji Emmanuel Adebayor ambaye sasa hana timu...,

 

Pamoja na kutokuwa na timu, Adebayor ameendelea kukomba kitita cha pauni 100,000 kila wiki kutoka Tottenham Hotspur.

Kwa kuwa fedha inaingia Adebayor ametupia mtandaoni akionyesha picha ya saa zake 12 za kthamani kubwa. Saa hizo jumla yake ni pauni 450, 000.
 

Katika manent aliyoandika, Adebayor anaandika hivi: “Wenye chuki watachukia, lakini hii ndiyo hali halisi.”

Kauli zake zimekuwa zikionyesha kuwadhi Waingereza ambao wanaona anachukua fedha za bure Spurs.



Lakini wanasahau ndiyo hali halisi ya mkataba, kweli wanachukia lakini ndiyo hali halisi.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget