Halloween Costume ideas 2015
Latest Post

katika miji mbalimbali walijitokeza kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2016 kwa njia mbalimbali. Huu hapa ni mkusanyiko wa picha za hali ilivyokuwa.
Australia ilikuwa moja ya nchi za kwanza kuingia mwaka 2016, fataki zinaonekana hapa juu ya jumba la Opera House na daraja la Harbour Bridge.

Sydney
Mjini Sidney


Nchini Misri, fataki zinaonekana zikilipuka karibu na Piramidi.
Cairo
Cairo Misri

Jijini Berlin, fataki zilitawala anga kama inavyoonekana hapa juu ya Lango la Brandenburg mjini Berlin.
Berlin
Mjini Berlin

Mjini London, hivi ndivyo hali ilivyokuwa karibu na Big Ben. Maelfu ya watu walijitokeza kutazama fataki.
London
London Uingereza

Mji wa Baghdad haukuachwa nyuma, na hapa fataki zinaonekana zikilipuka katika Bustani ya Zawra.
Baghdad
Mjini Bagdad

Mjini Singapore, mwaka mpya ulikaribishwa kwa fataki. Hapa ni Marina Bay.
 
Singapore
Mjini Singapore
 
 
Mjini Kuala Lumpur, nchini Malaysia fataki zinaonekana zikilipuka karibu na jengo mashuhuri ya Petronas Towers.
Mjini Kuala Lampur
Mjini Taipeni, Taiwan, fataki zinaonekana kwenye jumba refu la Taipei 101.
Taipei
Mjini Taipei, Taiwan
 
Mjini Paris, watu walikusanyika Champs Elysees kutazama video ya Mwaka Mpya iliyoonyeshwa katika Arc de Triomphe.
Paris
Mjini Paris, Ufaransa.
Nchini India, mwanamume huyo alitumia nyanya, vitunguu na pilipili kuandika 2016.
Nyanya
Mjini Amristar, India
Mjini Auckland, New Zealand fataki zililipuliwa katika jumba la Auckland Sky Tower, mkesha wa Mwaka Mpya

Fataki New Zeland

Hapa, mwanamume anaonekana akitembea karibu na mapambo yaliyoandika 2016 katika mji wa Kiev, nchini Ukraine. GDP ya taifa hilo ilishuka asilimia 9 mwaka 2015.
Kiev
Mjini Kiev
Mjini Brazil, baadhi waliamua kufika katika ufuko wa Copacabana mjini Rio de Janeiro kuukaribisha mwaka mpya.
 
Brazil
Mjini Rio
Mjini Beijing watu wengi waikusanyika kwa hafla iliyokuwa Hekalu la Tai Miao karibu na Forbidden City mjini Beijing.
Beijing
Mjini Beijing

Baraza la Mitihani la Tanzania limekuwa likipigiwa simu na watu mbalimbali wakiomba ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa limebadilisha Viwango vya Ufaulu (Grade Ranges).
 
Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha watahiniwa na umma kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni za UONGO na zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki.
 
Hivyo, Baraza linaomba umma kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa Baraza halijafanya mabadiliko yoyote kuhusu Viwango vya Ufaulu vinavyotumika sasa.
Imetolewa na,
AFISA HABARI NA UHUSIANO




katika kuukaribisha Mwaka Mpya maeneo mbalimbali yamekua na Shamra Shamra za aina yake huku kila mmoja akitaka kuonesha furaha yake katika kuvuka mwaka 2015 na kuelekea Mwaka 2016. 

Camera yetu ilinasa matukio kadhaa ya Kuufunga mwaka maeneo mbalimbali na hapa iliweza ibukia katika Jiji la Arusha na kukuta Sherehe ya aina yake huku watu wakisherehekea Kuingia Mwaka Mpya.


 

Katika Hafla hiyo iliyoshehena Vinywaji, Vyakula na Muziki ilihudhuriwa na watu mbalimbali kutoka Moshi na Arusha akiwemo Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema. Mh. Davis Mosha hakusita kuonesha furaha yake pale Mwaka Mpya wa 2016 ulipoingia kwa kushukuru Jamaa na MArafiki walioamua kuungana na familia yake katika kuuaga Mwaka Mpya.

 

"Ninashukuru familia yangu kwa kuandaa chakula na vinywaji leo na kujumuika pamoja nanyi katika siku hii, Naamini wakati huu mngekua katika maeneo yenu ili kuukaribisha mwaka lakini mmeamua kuja kuungana na familia yangu na tumeweza kuuaga mwaka Pamoja." Alisema Davis Mosha.

Tazama Picha zaidi za sherehe hiyo.


Chief  Mandara akiwa katika tafrija ya kukaribisha mwaka mwaka






MSOSI  TIME
Waalikwa wakipata Chakula

Mpigana Masumbwi wa Siku nyingi Hendrew mwenye koti jeusi akipata chakula.




Mke wa Mh. Davis Mosha Akipata Chakula katika Hafla ya kuuaga Mwaka







  MUZIKI TIME








 





Picha na Malaika









Diana Isaya akipokea cheti kutoka kwa Meneja wa huduma kwa jamii, Hawa Bayumi baada ya kuhudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Dar Live Dar es Salaam. Kulia ni Meneja mauzo wa Airtel, Fadhili Mwasyebya na mkufunzi wa mafunzo hayo Allen Mwangwele. (Na Mpigapicha Wetu).
Diana Isaya akipokea cheti kutoka kwa Meneja wa huduma kwa jamii, Hawa Bayumi baada ya kuhudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Dar Live Dar es Salaam. Kulia ni Meneja mauzo wa Airtel, Fadhili Mwasyebya na mkufunzi wa mafunzo hayo Allen Mwangwele.


VIJANA wametakiwa kuzigeuza changamoto zilizopo kwenye maeneo yao kwa kuzifanya kuwa fursa kwao na kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa na kubaki wakilalamika kuwa hakuna ajira...,


 

Pamoja na fursa hizo vijana pia wametakiwa kuitumia mitandao ya kijamii kutengeneza mifumo ya kibiashara kwa kubadilishana mawazo badala ya kutumia muda mwingi mitandaoni kujadili mambo yasiyo na tija.
Rai hiyo ilitolewa jana na Meneja wa Huduma za Kijamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Hawa Bayumi katika semina ya Airtel Fursa Tunakuwezesha inayotolewa Dar es Salaam kwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 na 24 ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea.

Alisema lengo la semina ni kuwapatia vijana waishio Dar es Salaam mafunzo ya biashara ya ujasiriamali kuweza kumudu uendeshaji biashara zao na mahitaji yao. Bayumi alisema: “Tumeamua kulenga kundi la vijana hawa kutokana na nguvu ya kundi hilo ambalo linauwezo wa kuleta mabadiliko makubwa kiuchumi iwapo litawezeshwa kupata elimu ya ujasiriamali”.

Mmoja wa wanufaika mjasiriamali Diana Isaya alisema kuwa amepata muongozo mzuri utakaokuza biashara zake na kuzifanya kwa weledi mkubwa zaidi. “Napenda kuwahimiza vijana wenzangu kuandaa mawazo ya biashara bila kusubiri kuwa na fedha ndiyo waanze kujipanga na kuchangamkia fursa zilizopo kwenye maeneo yao,” alisema Isaya.

Tangu kuanza kwa mafunzo hayo ya ujasiriamali kwa vijana, zaidi ya mikoa 10 imefikiwa ambapo vijana wengi wamenufaika na mpango huo na kuanzisha ama kuendeleza biashara zao.


WAKATI mdau wa Simba, Mohamed Dewji akionesha nia ya kutaka kuwekeza katika klabu hiyo kwa Sh bilioni 20, uongozi wa Simba bado unajivuta kutoa maamuzi huku ukiweka mambo sawa kuwa timu hiyo haiuzwi...,


 

Dewji alitangaza kwenye chombo kimoja cha habari kuwa siku ya leo itakuwa ni mwisho akiutaka uongozi wa Simba kutoa majibu, kama yeye aweza kufanya uwekezaji huo na kuanza mara moja utekelezaji wa mikakati yake kuanzia Januari mwakani.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari juzi, msemaji wa Simba, Haji Manara alisema uongozi wa klabu hiyo haupingi uendeshaji wa klabu katika mfumo wa kisasa isipokuwa wanahitaji kuwa makini.
“Hakuna taasisi, mtu, kikundi aliyeleta barua kutaka kuinunua Simba mpaka hivi sasa, hatuna. Ni suala ambalo wanachama wanahitaji kuelimishwa kwanza kabla ya kuingia huko,”alisema.

Kwa mujibu wa taarifa za Dewji, anataka kuwekeza katika klabu hiyo kwa nia ya kuiendesha kibiashara.
Alisema alikutana na viongozi wa Simba, Rais Evans Aveva akiwa na Kassim Dewji na Musley Ruhwehi na kuwaeleza dhamira yake lakini anaona viongozi hao hawako tayari.

Pia, alisema iwapo ataruhusiwa kufanya uwekezaji huo atajenga kiwanja cha Bunju na kuwa kiwanja maalum cha mazoezi ya klabu hiyo na pia kama kituo maalum cha kulea vipaji vya soka kwa vijana ambao baadaye watachezea timu hiyo.

Dewji alisema iwapo leo halitatoka jibu kuwa uwekezaji huo ataachana nao na kuendelea na shughuli zake.
Hata hivyo, Rais wa Simba Aveva hivi karibuni alisema suala hilo haliwezi kuamuliwa haraka, kuna mchakato wa kupitia katiba na kufanyia marekebisho lakini pia kuwahusisha wanachama kwenye mkutano mkuu kisha waridhie ndipo jibu liweze kutoka.


Rais Barack Obama wa Marekani amepanga kuitembelea rasmi Ujerumani mwishoni mwa mwezi wa April mwakani.Kwa mujibu wa ikulu ya Marekani mjini Washington, rais Obama atakutana mjini Berlin na kansela Merkel na kuwa rais wa kwanza wa Marekani kutembelea maonyesho makubwa kabisa ya kimataifa ya viwanda mjini Hannover, kaskazini mwa Ujerumani...,


 



Duru za Marekani zinasema rais Obama ataitumia ziara yake nchini Ujerumani kutetea makubaliano  ya biashara huru kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani-TTIP. Rais Barack Obama amedhamiria kutia saini makubaliano hayo,kabla ya mhula wake kumalizika mwaka 2017-makubaliano yatakayoanzisha kanda mojawapo kubwa kabisa ya biashara huru ulimwenguni.

Wengi wa wakaazi wa pande mbili za bahari ya Atlantik wanahofia makubaliano hayo yakitiwa saini vizuizi vya forodha vitaondolewa na kuzidishiwa nguvu na makampuni makubwa makubwa dhidi ya yale ya ndani pamoja na kukiukwa taasisi za kidemokrasi.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget