Staa wa R&B wa Marekani Chris Brown amekuwa haishiwi headlines..baada ya matukio mfululizo yakimuhusisha na Polisi, headlines zimerudi tena kwake.
Ukiachia lile tukio la kumpiga mwanamuziki mwenzake Rihanna mwaka 2009 na kutakiwa kutojihusisha na kosa lolote kwa miaka mitano hili ni tukio lingine lilolomrudisha kwenye mikono ya polisi huko Las Vegas.
Jana jumamosi akiwa katika klabu ya The Palms Casino Resort staa huyo anadaiwa kumpiga usoni mama mmoja Liziane Gutierrez ambaye alikua akijaribu kumpiga picha.
Polisi katika jiji la Las Vegas, Marekani bado wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na malalamiko ya mama huyo
Mwaka 2009, Brown aliagizwa kukaa miaka mitano bila kufanya kosa baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga nyota wa muziki wa pop Rihanna.
Post a Comment