katika kuukaribisha Mwaka Mpya maeneo mbalimbali yamekua na Shamra Shamra za aina yake huku kila mmoja akitaka kuonesha furaha yake katika kuvuka mwaka 2015 na kuelekea Mwaka 2016.
Camera yetu ilinasa matukio kadhaa ya Kuufunga mwaka maeneo mbalimbali na hapa iliweza ibukia katika Jiji la Arusha na kukuta Sherehe ya aina yake huku watu wakisherehekea Kuingia Mwaka Mpya.
Katika Hafla hiyo iliyoshehena Vinywaji, Vyakula na Muziki ilihudhuriwa na watu mbalimbali kutoka Moshi na Arusha akiwemo Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema. Mh. Davis Mosha hakusita kuonesha furaha yake pale Mwaka Mpya wa 2016 ulipoingia kwa kushukuru Jamaa na MArafiki walioamua kuungana na familia yake katika kuuaga Mwaka Mpya.
"Ninashukuru familia yangu kwa kuandaa chakula na vinywaji leo na kujumuika pamoja nanyi katika siku hii, Naamini wakati huu mngekua katika maeneo yenu ili kuukaribisha mwaka lakini mmeamua kuja kuungana na familia yangu na tumeweza kuuaga mwaka Pamoja." Alisema Davis Mosha.
Tazama Picha zaidi za sherehe hiyo.
Chief Mandara akiwa katika tafrija ya kukaribisha mwaka mwaka |
MSOSI TIME
Waalikwa wakipata Chakula |
Mpigana Masumbwi wa Siku nyingi Hendrew mwenye koti jeusi akipata chakula. |
Mke wa Mh. Davis Mosha Akipata Chakula katika Hafla ya kuuaga Mwaka |
MUZIKI TIME
Picha na Malaika |
Post a Comment