|
Familia ya Davis Mosha wakiwa kanisani katika Ibada ya Shukrani. |
Wananchi wa Moshi wameonekana kuvutiwa sana Aliyekua mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi jimbo la Moshi Mjini na Mfanyabiashara Mkubwa Mmiliki wa Kampuni ya Kampuni ya Delina General Enterprises Ndugu. Davis Elisa Mosha. Hayo yametokea anzia siku ya sikukuu ya Maulid ya waislam baada ya Mosha kualikwa na waislam wa Mkoa wa Kilimanjaro kuungana nao katika Kuadhimisha siku hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kila mmoja alieleza kwa hisia tofauti juu ya Davis kwa jinsi alivyokua na Roho ya kipekee lakini pia jamii kuona uthamani wake bila kujali dini itikadi wala kabila. Akizungumza huku akiwa na uso wa Furaha mmoja wa waumini wa kiislam alisema “Huyu bwana Mungu kaamua kumtumia na kila jambo Mungu hufanya kwa kusudi lake, Amewahi kusaidia uislam katika Maeneo mbalimbali ikiwemo kujenga Misikiti pamoja na kupeleka ma Shekh wetu Makha kwa Hijja, Lakini pia amekua akisaidia Masikini na katika Dini ya kiislam tunafundishwa kutoa Sadaka na moja ya sadaka bora ni kusaidia wasiojiweza. Nachoweza sema huu ni Mpango wa Mungu” Alimaliza kusema Shekh Ally Mtangi wa Mabogini.
|
Davis Mosha akiwa rafiki zake pamoja na Baadhi ya Mashekh wa kilimanjaro wakipata chakula siku ya Maulid. |
Pia Davis Mosha kila mwaka kwa zaidi ya miaka ishirini sasa hushiriki sikukuu ya Christmass na wakazi wa moshi huku akihakikisha anafanya familia zisizojiweza kuweza kufurahia sikukuu hiyo. Kila mwaka hutoa Mchele, Sukari, Sabuni na Kiasi cha Shilingi elfu hamsini kwa ajili ya kununulia nyama na mahitaji mengine kwa ajili ya sikukuu na vitu hivyo hutoa kwa Wazee, Wajane, Yatima na Walemavu na kila mwaka hutoa kwa watu mia tano na kila mmoja hupata vitu hivyo na kiasi hicho cha fedha. Sikukuu ya Christmass hii aliweza kushiriki misa ya Sikukuu na familia yake katika kanisa na kilutheri usharika wa kiboriloni na kuweza kutoa msaada huo kwa makundi hayo ambayo yalikuja kanisani hapo. Tuliweza kuzungumza na Mmoja wa Wazee ambao hunufaika na zawadi hiyo ya sikukuu kutoka kwa Familia ya Davis Mosha alisema haya. “sasa ni mwaka wa tisa mimi kuhudhuria tokea huyu kijana aanze kutuletea chakula na pesa za sikukuu, kila mwaka tunakuja hapa na anatusaidia kweli Mungu ambariki kijana huyu” Alisema Bibi Temu.
|
Davis Mosha akiposalimiana na wakazi wa Moshi baada ya kutoa zawadi ya Sikukuu. |
Naye Arold Mushi mkazi wa kiboriloni alisema hajawahi kukutana na binadamu mwenye roho kama ya Davis na wakati mwingine anaumizwa na watu ambao wanakwamisha juhudi zake na anachoamini Mungu ndiye kamtuma na kampa uwezo ili asaidie. “Huyu kijana wakati wake utafika tu wa kupewa nafasi ya kuongoza” Alimaliza Ndugu Mushi.
|
Mmoja wa wazee akiwa amepokea zawadi yake ya sikukuu toka kwa Mrs. Davis Mosha anayefahamika zaidi kwa jina la Madame Nance. |
Katika kumalizia sikukuu baada ya kula sikukuu nyumbani kwake Arusha pamoja na Rafiki na jamaa zake, Familia ya Davis Mosha iliandaa Tafrija katika Kata ya Njoro Mjini Moshi siku ya Tarehe 26 Disemba kwa ajili ya wakazi wa Moshi. Davis Mosha alisema
“Wananchi wa Moshi wapo Moyoni mwangu, Ni wakarimu sana na wamekua Ndugu zangu. Nimeishi nao kwa takribani miezi mitatu tukishirikiana katika matukio mbalimbali ya kijamii. Naelewa changamoto zinaowakabili, Naelewa maisha halisi wanayoishi na nafahamu wanahitaji kuwekwa pamoja na kutatua yale yanayowakabili kwa umoja wao, Niliwaahidi sitowaacha nitakua nao katika wakati wote wa shida na Raha. Leo nimekuja hapa kama Davis Mosha, Kama Ndugu yao. Siasa haijanileta hapa nimekuja kufurahia sikukuu pamoja nao. Nimeona si busara mimi na familia yangu kwenda mbali kula sikukuu na kuacha watu wenye upendo wa dhati nasi. Nawapenda sana watu wa Moshi” Alisema Mh. Davis Elisa Mosha.
|
Davis Mosha akiwa na baadhi ya Rafiki zake katika hafla ya sikikuu nyumbani kwake Arusha |
|
Davis Mosha na Rafiki zake kutoka Moshi katika hafla ya sikukuu nyumbani kwake Arusha |
|
Walemavu wakipata chakula katika hafla ya sikukuu iliyoandaliwa na Davis Mosha mjini moshi. |
Hata hivyo wakazi wa Moshi walifurahishwa sana na kitendo cha Mosha kuandaa tafrija hiyo kwa ajili yao bila kujali itikadi, Dini, Kabila wala chama na kuonekana waziwazi kujutia kumpoteza Davis katika kipindi alichoomba ridhaa ya kuwaongoza katika jimbo la Moshi Mjini.
|
Wakazi wa Moshi wakiwekewa chakula katika hafla ya sikukuu iliyoandaliwa na Mh. Davis Mosha Mjini Moshi. |
Post a Comment