Halloween Costume ideas 2015

OBAMA ATAWASILI HANNOVER MWEZI APRILI


Rais Barack Obama wa Marekani amepanga kuitembelea rasmi Ujerumani mwishoni mwa mwezi wa April mwakani.Kwa mujibu wa ikulu ya Marekani mjini Washington, rais Obama atakutana mjini Berlin na kansela Merkel na kuwa rais wa kwanza wa Marekani kutembelea maonyesho makubwa kabisa ya kimataifa ya viwanda mjini Hannover, kaskazini mwa Ujerumani...,


 



Duru za Marekani zinasema rais Obama ataitumia ziara yake nchini Ujerumani kutetea makubaliano  ya biashara huru kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani-TTIP. Rais Barack Obama amedhamiria kutia saini makubaliano hayo,kabla ya mhula wake kumalizika mwaka 2017-makubaliano yatakayoanzisha kanda mojawapo kubwa kabisa ya biashara huru ulimwenguni.

Wengi wa wakaazi wa pande mbili za bahari ya Atlantik wanahofia makubaliano hayo yakitiwa saini vizuizi vya forodha vitaondolewa na kuzidishiwa nguvu na makampuni makubwa makubwa dhidi ya yale ya ndani pamoja na kukiukwa taasisi za kidemokrasi.

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget