Waziri wa haki wa Afrika Kusini amefutilia mbali ombi la kutaka kesi inayomkabili mfalme wa jamii ya Nelson Mandela ya Thembu isikizwe upya.
Mfalme huyo , Buyelekhaya Dalindyebo alipatikana na hatia ya kushambulia watu , uteketezaji wa mali na kuhujumu mkondo wa sheria.
Makosa yake yanahusishwa na dhulma dhidi ya raia aliokuwa akitawala miaka ya 90, kwenye shamba alilomiliki mashariki mwa mji wa Cape.
Mfalme huyo aliteketeza nyumba za wapangaji watatu, akitaka kuwafukuza, kwa madai kuwa walikiuka sheria za jamii yao. Pia, alishambulia watu watatu hadharani kwa madai ya uhalifu.
Mahakama nchini Afrika ya kusini ilimhukumu kifungo cha miaka 12 gerezani.
Badala ya kujikibadhi kwa mamlaka, mfalme huyo wa aba Thembu, aliwasilisha ombi kwa mahakama, akisema kuwa hakuhukumiwa kwa haki.
Hata hivyo ombi lake limekataliwa hii leo jumanne, na waziri wa mahakama Michael Masutha, kwani hakutoa ushahidi mpya.
Mfalme huyo amesema kuwa hatokubali uamuzi huo, na anataka muda wa dhamana yake uongezewe.
Post a Comment