Halloween Costume ideas 2015

EL NINO YA MWAKA 98 KUJIRUDIA TENA YASEMA NASA..!!

 

                   

Je unakumbuka Hali ya hewa ya El Nino iliyowahi kutokea na kusababisha maafa makubwa katika nchi za Afrika ikiwemo Tanzania na Kenya. Mvua kubwa iliyobatizwa jina la El Nino kutokana na hali ya hewa hiyo iliikumba Tanzania na Kenya kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati na kusababisha maafa makubwa huku ikiwaacha wananchi bila makazi baada ya nyumba zao kusombwa na Mafuriko makubwa ya maji yaliyotokana na mvua hiyo....,




Hali ya hewa ya El Nino ambayo imekuwa ndiyo kali zaidi katika historia itazidisha hatari ya njaa na maradhi kwa mamilioni ya watu duniani 2016, mashirika ya misaada yamesema.

Hali hii ya hewa inatarajiwa kusababisha ukame baadhi ya maeneo na mafuriko kwingine.
Baadhi ya maeneo yanayotarajiwa kuathirika sana yako Afrika, huku uhaba wa chakula ukitarajiwa kufikia kilele Februari.

Maeneo mengine yakiwemo Caribbea, Amerika ya Kati na Amerika Kusini yataathiriwa katika kipindi cha miezi sita ijayo.

Hali ya hewa ya El Nino, hutokana na kuongezeka kwa joto na huathiri hali ya hewa maeneo mengi. Mwaka huu hali hii imezidi na kuufanya mwaka 2015 kuwa mwaka wenye joto zaidi duniani katika historia.
Kufikia sasa, watu 31 milioni wanakabiliwa na uhaba wa chakula Afrika, theluthi moja kati ya hawa wakiwa Ethiopia.
Inakadiriwa kwamba watu 10.2 milioni watahitaji chakua cha msaada mwaka 2016.

"Tukikosa kuchukua hatua sasa, tutahatarisha zaidi maisha ya watu wasio na uwezo maeneo mbalimbali duniani,” waziri wa ustawi wa kimataifa Uingereza Nick Hurd amesema kupitia taarifa.

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget