Halloween Costume ideas 2015

WAZIRI ATOA WIKI MBILI KWA WALIOJENGA MABONDENI KUHAMA

 
Serikali imesitisha zoezi la bomoabomoa kwa muda wa siku 14 ili kuwapa muda wa kutosha watu waliovamia na kuishi katika bonde la Mto Msimbazi Mkwajuni kuondoka, ambapo imesisitiza kuwa baada ya siku hizo kuisha zoezi hilo litaanza tena na hivyo wahakikishe wanaondoka  wenyewe.

Akitoa tamko hilo waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh William Lukuvi amesema waliojenga katika eneo hilo wapo hapo  kinyume na sheria  kwa sabubu ni mahali hatarishi.
 Akaongeza kuwa kuanzia mwakani wizara yake itagawa kwa viongozi wa serikali za mitaa ramani za mipango miji ili waweze kuzisimamia kwa ukaribu ili kuepusha uwezekano wa kutokea ama kufanya ujezi holela.
 
Aidha baadhi ya wananchi wamepongeza zoezi za bomoabomoa na kusema kuwa imekuwa na hatua ngumu lakini muhimu kwani eneo hilo limekuwa likisababisha vifo vya watu kila mafuriko yanapotokea hivyo watu kuondolewa hapo wamenusurishwa kwa mengi.
 
Katika hatua nyingine waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Mh Jenister Mhagama ameziagiza kamati za maafa katika ngazi za mikoa, wilaya na vijiji kuorodhesha na kuwapa barua za kuwataka watu wote wanaoishi maeneo hatarishi kuhama mara moja katika maeneo hayo na utekelezaji wa agizo hilo uwasilishwe ofisi ya waziri mkuu haraka iwezekanavyo.
Labels:

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget