Kocha wa klabu ya Chelsea Guus Hiddink |
Kocha Mpya wa klabu ya Chelsea Guus Hiddink amesema kuwa ana wasiwasi mkubwa sana juu ya nafasi ambayo Chelsea wanaweza kukamata, huku akifurahishwa na hali ya wachezaji wake kujiamini baada ya suluhu katika mchezo wao dhidi ya Manchester United hapo jana.
Hiddink atadumu na Chelsea mpaka mwishoni mwa msimu huu baada ya aliyekuwa kocha Jose Mourinho – kufukuzwa Disemba 17 wakati Chelsea wakiwa juu kwa alama moja tu dhidi ya timu zilizo kwenye mstari wa kushuka daraja.
Akiongea baada ya mchezo dhidi ya Man Ubited, Hiddink alisema: “Bila shaka nina wasiwasi sana lakini nitakuwa na hofu zaidi kama wachezaji hawajiamini pamoja na kuwa na malengo”.
“Nina furaha kupata pointi hapa kwa sababu ya hali ngumu tuliyokuwa nayo kutokana na kukosekana kwa washambuliaji wetu wote wa kati Radamel Falcao, Loic Remy pamoja na Diego Costa ambaye alikuwa na kadi mbili za njano”, alisema Hiddink.
“Nia yetu ilikuwa ni kufunga magoli lakini kutokana na sababu mbalimbali, nina furaha na kiwango tulichoonesha”
Kuhusu suala la hatihati ya klabu hiyo kushuka daraja, Hiddink amesema kwamba: “Huwezi kusema kuwa hatuwezi kushuka daraja ila suala la muhimu ni kusonga mbele na kuweza kupata matokeo mazuri zaidi”.
Post a Comment