Waislamu wa dhehebu ya Shia kaskazini mwa Nigeria wameandamana kupinga operesheni wa kijeshi ambayo wanasema ilisababisha vifo vya mamia ya waumini.
Maandamano yalishuhudiwa katika miji sita mita mikuu, mji wa Kaduna ukiathirika zaidi.Rais wa Iran, Hassan Rouhani alimpigia simu mwenzake wa Nigeria Muhammadu Buhari kuhusu operesheni hiyo ya jeshi.
Iran ni taifa la Kishia.
Jeshi la Nigeria linatuhumu dhehebu hilo la Kishia kwa kujaribu kumuua mkuu wa jeshi Jenerali Tukur Buratai.
Dhehebu hilo kwa jina Islamic Movement of Nigeria (IMN), limekanusha madai hayo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran, kwenye mawasiliano yake na Bw Buhari, Bw Rouhani aliuliza kuhusu hatima ya Sheikh Ibraheem Zakzaky, kiongozi wa IMN aiyekamatwa baada ya wanajeshi kuzingira nyumba yake katika mji wa Zaria.
Dhehebu la IMN linasema mamia ya waumini wake waliuawa na wanajeshi na madhabahu ya kundi hilo yakaharibiwa kwenye operesheni ya kijeshi.
Mtetezi wa haki za kibinadamu Chidi Odinkalu, ameunga mkono takwimu zinazotolewa na kundi hilo na kumtaka Rais President Buhari kuunda tume huru ya uchunguzi
“Haiwezekani. Wanigeria wana haki ya kuishi. Jeshi linawezaje kukabili watu wanaoandamana wakirusha mawe kwa bunduki?” Bw Odinkalu ameongeza.
Kundi la IMN lina makao makuu yake IMN na wafuasi wa dhehebu hilo waliandamana, huku vikosi vya usalama vikishika doria.
Mwandishi wa BBC Nura Muhammed Ringim anasema watu wengi walisalia manyumbani wakihofia usalama.
Miji ya Kano, Katsina, Sokoto, Zamfara na Bauchi pia ilishuhudia maandamano.
Nchini Iran, kundi la watu lilikusanyika nje ya afisi za Umoja wa Mataifa mjini Mashhad kupinga maandamano hayo, kwa mujibu wa shirika la habari la kibinafsi la Tehran Tasnim.
Jeshi halijatoa idadi ya watu waliofariki, lakini limekanusha madai kwamba mkewe kiongozi huyo wa IMN Zeenat Ibrahim aliuawa.
Meja Jenerali Oyebado, mkuu wa jeshi wa Kaduna, alisema Jumatatu kwamba mwanamke huyo anazuiliwa na jeshi.
Hakuthibitisha wala kukana madai ya kuuawa kwa mwana wa kiume wa Sheikh Ibraheem Zakzaky, Sayyid Ibraheem Zakzaky.
Mwaka uliopita, wana watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky waliuawa kwenye makabiliano kati ya jeshi na wafuasi wa dhehebu hilo.
Post a Comment