Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United anayekipiga katika klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani kwa sasa Javier Hernandez Chicharito amefunguka kwa nini aliamua kuondoka Man United. Chicharito ambaye aliondoka Man United mwaka 2015 baada ya kucheza kwa mkopo wa muda mfupi ndani ya klabu ya Real Madrid.
Kwa mara ya kwanza Chicharito ndio anatajwa sababu ya iliyomfanya aondoke Man United. Sababu za mshambuliaji huyo hazitofautiani sana na wachezaji wengine walioondoka Man United kwa sababu ya kocha wa Louis van Gaal, Chicharito ana mtuhumu kuwa Van Gaal ndio aliyesabisha yeye kupoteza kujiamini na hatimae kundoka Man United.
Van Gaal aliniambia kuwa tayari ana washambuliaji wake , kitu kilichonifanya nipambane kutafuta namba ila hakunipa nafasi, uongozi uliniambia kuwa nitaenda kwa mkopo Real Madrid kitu ambacho kilikuwa kigumu kwangu, baadae nilihamia Bayer timu ambayo najihami nacheza na ninafuraha” >>> ChicharitoToka Louis van Gaal ajiunge na Man United wameondoka jumla ya wachezaji 22 ambao ni Nemanja Vidic (InterMilan), Patrice Evra (Juventus), Jonny Evans (WBA), Darren Fletcher (WBA), Tom Cleverly (Everton), Rafael da Silva (Lyon), Angelo Enriquez (Dinamo Zagreb), Will Keane (Preston), Adnan Januzaj (Loan-Dortmund), James Wilson (Brighton), Robin Van Persie ( Fenerbahçe), Danny Welbeck (Arsenal), Radamel Falcao (Chelsea), Angel di Maria (PSG), Luis Nani (Fenerbahçe), Anders Lindegaard (WBA), Shinji Kagawa (Dortmund), Micheal Keane (Burnley), Federico Macheda (Cardiff), Wilfried Zaha (Crystal Palace), Ben Amos (Bolton Wanderers), Tyler Blackett (Celtic).
posted by nick j
Post a Comment