Halloween Costume ideas 2015

CCM YAJIPANGA KWA UCHAGUZI ZANZIBAR


KAMATI Maalumu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein imewataka wananchi na wanachama kujiweka tayari na hatimaye kujitokeza katika uchaguzi mkuu wa marudio.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu, wananchi wametakiwa kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio na kuachana na propaganda zinazotolewa na watu wachache kwa lengo la kupotosha ukweli.

“Kikao cha Kamati Maalumu ya CCM Zanzibar kilichokutana hapa chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar, Dk Shein kimewataka wananchi, wanachama na wafuasi wa CCM kujitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa marudio ambao tarehe ya kufanyika kwake itatangazwa na taasisi husika,” imesema taarifa hiyo ya Waride.

Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25 ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha kwa kile alichoeleza ni kuwepo kwa ukiukwaji wa kanuni na sheria za uchaguzi huru wa kidemokrasia.

Katika kikao cha jana kilichohudhuria pia na viongozi kadhaa wa kitaifa akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kilijadili ajenda mbili ikiwemo hali ya kisiasa mara baada ya uchaguzi mkuu kwa upande wa CCM.

Katika taarifa hiyo, chama hicho kimesema kimeridhishwa na mwenendo wa hali ya kisiasa na kimewapongeza wanachama waliojitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

Aidha chama kimepongeza na kutoa baraka kwa mazungumzo yanayoendelea ya viongozi wakuu wa kisiasa yakiwa na lengo la kuleta amani ya kudumu. Kamati ya mazungumzo ya hali ya kisiasa Zanzibar yenye lengo la kusaka amani ya kudumu iliyovurugika kutokana na kufutwa kwa uchaguzi mkuu inaundwa na viongozi wastaafu wakiwemo marais, Dk Salmin Amour, Amani Abeid Karume, Balozi Seif Ali Iddi ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Seif Sharif Hamad na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.

Akizungumza juzi Ikulu, jijini Dar es Salaam, Rais wa Zanzibar, Dk Shein alisema mazungumzo hayo yanaendelea vizuri na taarifa kamili yatakapofikia tamati. Alipoulizwa kuhusu hatma ya CCM kama uchaguzi mkuu utarudiwa, Waride alisema chama bado kiko imara na hakijatetereka.

“Wapo wanaosema CCM imeyumba, si kweli wala CCM haijapoteza majimbo kwa sababu kura hazikumalizwa kuhesabiwa,” alisema.
 www.africaswahilimedia.blogspot.com
Labels:

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget