Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) limewafungia Michel Platini na Sepp Blatter kujihusisha na shughuli zozote za soka kwa kipindi cha miaka 8.
Sepp Blatter ambaye alikuwa Rais wa Shirikisho hilo kabla ya kujiudhulu wadhiwa huo mwezi wa sita mwaka huu na Michel Platini akiwa Makamu wake. Wamehukumiwa kutokana na kukutwa na hatia ya kukiuka maadili ya shirikisho hilo kwa kuhusika na kupokea rushwa na matumizi mabaya ya ofisi ,ambapo Kubwa zaidi ni malipo yaliyojaa utata (dola milioni 2 za Kimarekani) aliyopokea Platini mwaka 2011 yaliyoidhinishwa na Blatter.
Hata hivyo FIFA kupitia kamati yake ya maadili inayoongozwa na jaji Hans-Joachim Eckert imewalima faini viongozi hao ambapo Blatter amelimwa faini ya dola 33,700 wakati Platin amepigwa faini ya dola 53,940 kama sehemu ya adhabu hiyo
Hii ina maana kuwa ndoto za Rais wa UEFA ambaye pia ni makamu wa Rais wa FIFA.Michael Platin za kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi wa shirikisho hilo uliopangwa kufanyika mwakani mwezi wa pili imeota mbawa kutokana na kutakiwa kutojihusisha na soka katika kipindi chote cha miaka 8 kuanzia leo
Aidha hali kama hiyo pia inamkuta Blatter ambaye alikuwa na tumaini la kuachiwa huru katika kifungo cha awali cha siku 90 ili ashiriki katika utoaji wa tuzo za mwanasoka bora wa dunia za Ballon D’or.
Hata hivyo taarifa zinasema kuwa viongozi hao wamepewa nafasi ya kukata rufaa kama wanaona hawajatendewa haki na kamti hiyo huru ya maadili.
Post a Comment