|
Wachuuzi nchini Zimbabwe wakisubiri wateja wa nguo. |
ZIMBABWE
Uchumi wa Zimbabwe unamalizika mwaka huu ukibashiriwa kuwa bei zitaendelea kushuka mwakani. Lakini wachumi wanasema mwenendo huo huenda usimnufaishe mtu yeyote.
Wazimbabwe wengi wanaonekana kuwa katika hali mbaya zaidi leo kuliko hapo mwaka 2009, pale taifa hilo la kusini mwa Afrika lilipoachia sarafu yake isiyo na thamani na kuanza kutumia sarafu mbali mbali hususan dola ya marekani. Baada ya miaka ya mfumuko mkubwa wa bei, bei sasa zimetulia na mambo yanaonekana kubadili mwendo. Sasa kuna kushuka kwa bei nchini Zimbabwe.
Lakini John Robertson,mchumi huru hapo mjini Harare anaeleza kuwa hizo si habari njema, kwa wazimbabwe wala kwa serikali ya rais Robert Mugabe.
Robertson anasema, kushuka kwa bei kwa kawaida kunahusishwa na watu kuwa na fedha za kutumia, lakini kuchaguwa kutonunuwa kile wanachokitaka kwa sababu kitakuwa rahisi zaidi mwezi ujao au baada ya miezi miwili au mitatu. Kile kilichokuwa kikipunguka nchini Zimbabwe ni rai ya ununuzi. Mishahara ya serikali inalipwa kutokana na pato la kodi ya serikali na pato hilo linashuka. Kwa hiyo serikali haina uwelewa wa maendeleo kwenye masoko.
Robertson anasema kutokana na mapato na hali ya kiuchumi, serikali inapaswa kupunguza shughuli zake. Kwa vile haijafanya hivyo, Robertson anasema hilo linaeleza kwa nini serikali ya Mugabe haiwezi kuwalipa wafanyakazi wake mishahara mwezi huu. Pato linapunguka, lakini idadi ya wafanyakazi inaongezeka. Wafanyakazi wa serikali wanatumia Zaidi ya asli mia 85 ya pato yanayokusanywa.
Gift Mugano, mdhahiri mwandamizi wa uchumi katika chuo kikuu cha Zimbabwe, na ni mshauri wa serikali. Anaelezea safari ya Zimbabwe ya mfumuko mkubwa wa bei na kushuka kwa bei. Anasema hali zote za kiuchumi zimesababisha mashaka kwa wazimbabwe wengi. Sehemu ya tatizo ni udhaifu wa Rand ya Afrika kusini na Kwacha ya Zambia, ambazo zimepelekea kupunguzwa kwa bei za bidhaa Zimbabwe inazonunua kutoka nchi hizo mbili.
Kwa hiyo huko nchini Zimababwe, kulikuwa hakuna bidhaa za kununuliwa mwaka 2009, hivi sasa hakuna fedha za kununuwa bidhaa zilizopo pale mwaka 2015 unapomalizika. Wote Mugano na Robertson wanasema kuna haja ya kubuni uwekezaji ili kuwa na wigo mpana wa mapato na ajira nchini Zimbabwe ili kushughulikia suala la kushuka kwa bei.
Post a Comment