Leo Disemba 23 katika Duru la Michezo magazetini tumeweza kukuletea yale waandishi na wahariri waliona yafaa kuwapasha kupitia magazeti. Nakuletea Habari Tano zilizopewa uzito katika Magazeti leo ya Tanzania.
5- Majabvi amalizana na Simba (Championi)
Habari za kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe anayeichezea Simba Justice Majabvi amemalizana na uongozi wa klabu hiyo baada ya kugoma kwa siku kadhaa kuungana na timu hadi atimiziwe baadhi ya mahitaji muhimu kama nyumba ya kukaa na kudai kuchoka kukaa hotelini. Habari ni kuwa Majabvi anaenda Shinyanga kuungana na timu na ameagizwa aandike barua ya kuomba msamaha“Mambo yako pouwa sasa, Majabvi alikutana na baadhi ya viongozi na mambo yamekwisha ila kaambia aandike barua ya kuomba msamaha”
4- CAF yamrejesha Dida golini Yanga (Championi)
Kocha wa makipa wa Yanga Juma Pondamali Mensah amethibitisha sababu za kumrejesha golini golikipa Deogratus Munishi Dida katika mechi za Ligi Kuu za African Sports na Stand United “Dida amepata namba tena kwa sababu nataka kumpa uzoefu, mimi sio kama makocha wengine ambao humuweka kipa mmoja tu msimu mzima, Yanga kwa sasa tunamichuano ya CAF hivyo kila kipa anatakiwa kucheza”
3- Kamusoko afifisha nyota ya Niyonzima (dimba)
Mashabiki wa Yanga wanaelekea kumsahau kiungo wao Haruna Niyonzima, na sasa mioyo yao wameipeleka kwa kiungo Mzimbabwe Thabani Kamusoko, kwa sababu Niyonzima amekuwa akiwazingua kwa siku za hivi karibuni na kuingia kwa Mzimbabwe huyo kumekuwa faraja kwao. Kwa sasa Niyonzima amefungiwa na Yanga kwa muda usio julikana kutokana na tabia ya utovu wa nidhamu ya kwenda kwao na kurudi wakati anaotaka.
2- Hat-trick ya Tambwe yamvuruga Maguli (LETE Raha)
Mshambuliaji wa Stand United na timu ya taifa ya Tanzania Elias Maguli, anaikunia kichwa kasi ya ufungaji ya Amissi Tambwe, lakini amesema hatishwi. Maguri anaongoza msimamo wa wafungaji magoli Ligi Kuu akiwa na jumla ya magoli 9, wakati Tambwe amefunga hat-trick dhidi ya Stand United na kufikisha jumla ya goli 8. “Kama nitakuwa uwanjani na sina nafasi ya kufunga nitampa pasi yule mwenye nafasi nzuri kwa faida ya timu, sitaki kumuangalia Tambwe au mwingine kafanya nini”
1- Samatta apata timu Ulaya (dimba)
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Mbwana Samatta amethibitisha kupata timu ya kwenda kucheza soka Ulaya na kuwa mipango yake inaenda vizuri“Siwezi kusema mengi, kilichopo ni kuwa mipango inaendelea na kwa jinsi mambo yanavyokwenda sina wasiwasi wa kwenda Ulaya kusaka ulaji mpya, kilichobaki ni kuomba uhai”
Post a Comment