Halloween Costume ideas 2015

LEICESTER CITY YAWAWEKEA KIZINGITI MANCHESTER CITY






UINGEREZA
               

Ikiwa ligi kuu Uingereza ikiwa inaendela kutimua vumbi wiki hii huku michezo kadhaa ikiwa imechezwa viwanjani jana huko Uingereza, Timu mbalimbali zimezidi kutambiana huku Leicester City ikiendelea kuonekana ni kizingiti kigumu kwa timu kubwa nchini Uingereza..,







Klabu ya Leicester City imeendelea kushangaza katika Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kutoka sare tasa na miamba Manchester City Jumanne.


Kutokana na sare hiyo, Leicester sasa wana alama sawa na viongozi wa ligi Arsenal, ingawa wako nambari mbili ukizingatia tofauti ya mabao.
Man City ndio waliotawala mchezo huo uliochezewa dimba la King Power kwa asilimia 61, huku wenyeji Leicester wakimiliki kwa asilimia 39 .

Leicester


Wachezaji wa Man City Aleksandar Kolarov, Kevin De Bruyne, Eliaquim Mangala walipewa kadi za manjano huku Marc Albrighton wa Leicester naye akipewa kati ya njano na mwamuzi Craig Pawson.


 

Ligi hiyo itaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa Paka Weusi wa Sunderland watawaalika majogoo wa jiji la Anfield katika dimba la Stadium of Light.

    

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget