WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema hana orodha ya majina ya watu wanaouza dawa za kulevya na hana muda wa kushughulika na hiyo inayoitwa orodha.
Badala yake, amesema chini ya uongozi wake ataweka mifumo itakayosaidia kudhibiti uingizaji wa dawa hizo nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kufanya kikao na maofisa wa ngazi ya juu wa Polisi, Kitwanga alisema wamekubaliana kuhakikisha dawa za kuleya zilizoko nchini zinakamatwa na kuteketezwa.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mh. Charles Kitwanga. (Picha kutoka Maktaba) |
Post a Comment