Kuweka akiba ni bora lakini maisha, kazi na dawa. Na ndicho ameonyesha mshambuliaji Emmanuel Adebayor ambaye sasa hana timu...,
Pamoja na kutokuwa na timu, Adebayor ameendelea kukomba kitita cha pauni 100,000 kila wiki kutoka Tottenham Hotspur.
Kwa kuwa fedha inaingia Adebayor ametupia mtandaoni akionyesha picha ya saa zake 12 za kthamani kubwa. Saa hizo jumla yake ni pauni 450, 000.
Katika manent aliyoandika, Adebayor anaandika hivi: “Wenye chuki watachukia, lakini hii ndiyo hali halisi.”
Kauli zake zimekuwa zikionyesha kuwadhi Waingereza ambao wanaona anachukua fedha za bure Spurs.
Lakini wanasahau ndiyo hali halisi ya mkataba, kweli wanachukia lakini ndiyo hali halisi.
Post a Comment