Kabla hajawa dj mkubwa Marekani na Duniani, Dj Khaled aliweza kuwapa nafasi ya kung’ara wasanii wakubwa kama Birdman,Lil Wayne na Mavado kwa kusambaza na kutangaza kazi zao mitaani.
Wazazi wa Dj Khaled walikuwa wasanii na walipendakufanya muziki wa kiarabu.
Khaled alikuwa na duka la muziki mjini New Orleans na mwaka 1993 alikutana na Birdman na Lil Wayne.
Khaled aliendelea na harakati za muziki mpaka kuja kuwa mtangazaji wa kipindi cha The Luke Show. Mwaka 2003 Khaled alianzisha kipindi chake cha radio WEDR.
Baada ya kuwa karibu na wasanii kwa muda mrefu Dj Khaled aliona ni nafasi nzuri kuwatumia wasanii hawa kutengeneza pesa ambazo zitawafaidisha wote na mwaka 2006 kuelekea 2008 Khaled aliwakutanisha wasanii wakubwa kwa mara ya kwanza na kutengeneza album ya Listennn… the Album and We the Best.
Post a Comment