MAREKANI YAWAKINGIA KIFUA WAANDISHI WA HABARI
Ikulu ya Marekani imeitaka Ethiopia iache kuitumia sheria inayotatanisha ya kupambana na ugaidi kama kisingizio cha kuwatia jela waandishi habari....,
Msemaji wa baraza la usalama wa taifa Ned Price hakuwataja waandishi habari hao waliotiwa ndani-hata hivyo ripoti yake imefuatia msako mkubwa wa Ethiopia dhidi ya wapinzani. Msemaji wa baraza la usalama wa taifa-Ned Price alisema,
"Tumeingiwa na wasi wasi mkubwa kutokana na kukamatwa waandishi habari wengine nchini Ethiopia."
Ikulu ya Marekani imeihimiza Ethiopia iwaachie huru waandishi wa habari hao na watu wengine waliofungwa kwasababu ya kutumia uhuru wao wa kujieleza.
Serikali ya Marekani imeitaka pia serikali ya Ethiopia-mshirika wake mkubwa barani Afrikla, iache kuitumia sheria ya kupambana na ugaidi kama chombo cha kuwanyamazisha wapinzani. Serikali ya mjini Addis Ababa imetakiwa ilinde haki za waandishi habari,wanablogi na wapinzani za kuandika na kuzungumza bila ya kipingamizi.
Post a Comment