RAIS wa awamu ya tano Dk. John Magufuli, ametoa zawadi ya vyakula, mbuzi na mafuta ya kupikia zenye thamani ya Sh mil 8,089, 000 kwa watu walio katika makundi maalum wakiwemo watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi,watu wenye ulemavu pamoja na wazee.
Akikabidhi msaada huo katika kituo cha kulelea watoto wanaokinzana na sheria kilichopo Upanga jijini Dar es Salaam, kwa niaba ya Dk. Magufuli, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Rabikira Mushi, alisema katika kusheherekea sikukuu za maulid,Chrismas na mwaka mpya Dk Magufuli ameamua kutoa zawadi katika vituo nane katika mkoa wa Dar es Salaam , viwili Zanzibar na Vituo Vitano toka mikoani kwa Tanzania Bara.
Alitaja vituo hivyo kuwa ni Makao ya Taifa ya watoto yatima Kurasini,mahabusi ya watoto Upanga kilichopo Ilala,Makao ya Wazee na wasiojiweza Nunge Kigamboni,Chuo cha Ufundi kwa watu wenye ulemavu Yombo, Kituo cha Mother Theresa Mburahati Kinondoni,Kijiji cha Furaha Mbweni kilichopo Kinondoni, Dar al arqum Tandika (Temeke) na kituo cha watoto Msimbazi, Kwa Zanzibar kituo cha Maboani Chakechake Pemba na Cha wezero Unguja.
Alisema kwa mikoa ya Tanzania Bara vituo vilivyopatiwa msaada ni Makao ya watoto Kemondo(Bukoba), Kituo cha Village of Hope(Dodoma),Shule ya maadirisho Irambo(Mbeya), Makazi ya wazee wasiojiweza Bukumbi,Misungwi(Mwanza) na Makazi ya wazee wasiojiweza Sukamahela, Manyoni, (Singida).
“Lengo la Dk. Magufuli kutoa zawadi hiyo ni kuwawezesha makundi hayo ya weze kusheherekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengine.”alisema Mushi.
Meneja wa mahabusu ya watoto Upanga, Ramadhani Yahaya alisema wanamshukuru rais Dk. Magufuli kwa ukarimu wake hasa kuwakumbuka watoto wa ukinzani wa sheria na kudai kuwa mara nyingi wadau wamekuwa hawawakumbuki.
“Tunawaomba wadau wengine wawe na moyo wa kuwasaidia watoto hawa, pia tuna matatizo ya ufinyu wa bajeti katika serikali kunahuduma muhimu ambazo tunazikosa tunaomba wadau mbalimbali wajaribu kusaidia kutujengea uzio kwakuwa serikali itachukua muda kutatua tatizo hilo”.alisema Mushi.
Post a Comment