Nyota wa Brazil atangaza nchi anayotaka kuhamia kwa ajili ya kuendeleza uchezaji soka
Kiungo wa kati wa Brazil Ronaldinho, amebainisha mpango wake wa kutaka kuhamia nchini Marekani kwa ajili ya kuendeleza uchezaji wake wa soka.
Ronaldinho ambaye kwa sasa ni mchezaji huru aliyeondoka Fluminense, ataendelea kuchezea kilabu hiyo mwezi ujao kwenye mashindano ya kombe la Florida Cup kwa mazingatio ya kipengele cha mkataba alitoa saini wakati wa kujiunga.
Ronaldinho mwenye umri wa miaka 35, alielezea matarajio yake ya kuhamia Marekani na kuendelea kucheza soka baada ya kumaliza mkataba na Fluminense.
Hata hivyo, Ronaldinho amesema kwamba atahitaji wiki kadhaa zaidi ili kuweza kufikiria zaidi mpango huo kabla ya kutoa uamuzi wake wa mwisho
Post a Comment