Halloween Costume ideas 2015

DAVIS MOSHA AHUDHURIA HAFLA YA MAULIDI KILIMANJARO

Gari aina ya Rolls Royce alikuja nalo Mkurugenzi wa Africa Swahili Media katika viwanja vya Bakwata Mkoa wa Kilimanjaro.
\
Mkurugenzi wa Kampuni ya Africa Swahili Media Ndugu Davis elisa Mosha leo amehudhiria Hafla ya chakula cha Mchana ya Maulidi Mkoa wa Kilimanjaro. Davis Mosha ambaye ni Mlezi wa Umoja wa Maimamu wa Mkoa wa Kilimanjaro ameweza kujumuika na Waislamu wa Mkoa wa Kilimanjaro katika chakula cha Mchana.

Mkurugenzi wa Africa Swahili Media Davis Mosha akiwa na Rafiki zake katika ofisi za Bakwata.


Kwa kawaida waislamu duniami kote husheherekea Maulid  ambayo ni sikukuu ya dini ya Uislamu ya kuzaliwa kwake Mtume Muhammad.
Neneo lenyewe ni la asili ya kiarabu kutokana na مولد النبي (maulid an-nabi) au (milaad an-nabi) ميلاد النبي . Sikukuu inafuata kalenda ya Kiislamu. Waislamu wa dhehebu la Sunnihusheherekea tar. 12 Rabi'-ul-Awwal na Waislamu wa dhehebu la Shia husheherekea tarehe 17. Rabi'-ul-Awwal. Muhammad alizaliwa takriban mwaka 570 BK.
Mkuurugenzi wa Africa Swahili Media wakipata Chakula leo Mchana.

Kutokana na kalenda hiyo usiku wa leo ndio siku ambayo waislam watasoma kisomo cha Maulid na kwa Mkoa wa Kilimanjaro Sherehe hizo za Maulid zinatarajiwa kufanyika katika Msikiti wa Riyadh uliopo kata ya Bondeni na Kiusa Mjini Moshi.
Mkurugenzi wa Africa Swahili Media wakipata chakula pamoja na Mashekh wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumza na Muandishi wetu Ndugu Davis Mosha ameshukuru kwa kupata mualiko wa kushiriki pamoja na waislam huku akisema anaheshimu Dini ya kiislam na amekua akiishi katika Misingi ya kiislam hata kufunga Ramadhani na kuhakikisha anajitoa katika kusaidia waislam sababu ni moja ya Dini ambazo zinahubiri amani na Umoja.

Labels:

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget