Halloween Costume ideas 2015

Kiongozi wa kundi la waasi auawa Syria

Kiongozi wa kundi moja kuu la waasi nchini Syria ameuawa kwenye shambulio la angani katika viunga vya mji wa Damascus.
Zahroun Alloush, ambaye ndiye mwanzilishi wa kundi la Jaysh al-Islam ameuawa pamoja na viongozi wengine wa kundi hilo, ripoti zinasema. Walikuwa mkutanoni waliposhambuliwa kwa kombora, wanaharakati wamesema.
Kundi hilo la wapiganaji huungwa mkono na Saudi Arabia na limekuwa likipigana katika maeneo ya karibu na mji huo mkuu wa Syria.
Majuzi lilijiunga na makundi mengine ya upinzani mjini Riyadh katika kuunda mkakati wa kufanikisha mazungumzo ya amani na serikali.
Hayo yakijiri, mabasi kadhaa yamewasili katika kambi ya wakimbizi ya Yarmouk nchini Syria, kabla ya kuanza rasmi wakati kuwaondosha wapiganaji waasi, wakiwemo wanachama wa kundi la wanamgambo wa Islamic State na familia zao.
Muda huo, ulifanikishwa na Umoja wa Mataifa ungali kufahamika, lakini runinga ya Hezbollah na kundi la kutetea haki za kibinadamu la Syrian Observatory, linasema kwamba mabasi 18 tayari yamefika huko kuwahamisha waasi hao kutoka katika kambi zao zilizozingirwa kusini mwa mji wa Damascus.
Watapewa ulinzi maalum, hadi waingie salama katika kambi yao kuu, iliyoko katika mji wa Raqqa.

by Nickson John
Labels:

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget