Rapa Drake ametajwa kuwania tuzo tano za Grammy mwaka huu kupitia nyimbo zake “Back to Back” na Best Rap Song for “Energy”ila lebel yake ya Cash Money ingeweza kuongeza namba ya tuzo anazowania mwaka huu.
Wimbo mmoja ambao watu wameshanga haujatajwa kwenye tuzo hizi ni wimbo wa “Hotline Bling,” wenye mafanikio kuliko “Back To Back” na “Energy” .
Hits Daily Double imetoa repoti kuwa lebel ya Cash Money haikupeleka wimbo huo kwenye tuzo hizo. Wimbo huu ungekuwepo kuna uwezekano ungeshinda “Record of the Year.”
Drake alishinda tuzo ya Grammy kwenye kipengele cha Best Rap Album mwaka 2012 kupitia album ya Take Care.
Post a Comment