Halloween Costume ideas 2015
Articles by "AFRIKA"

Maelfu ya watu wameandamana katika miji mikuu ya Afrika Kusini wakitaka kutimuliwa kwa Rais Jacob Zuma.
Wanasema visa vya ufisadi na mapendeleo vimeongezeka sana.
Makundi yaliyoandaa maandamano hayo yamekuwa yakitumia kitambulisha mada #zumamustfall kutafuta uungwaji mkono mtandaoni.
Maandamano hayo yamefanyika Siku ya Maridhiano, siku ya mapumziko ambayo lengo lake ni kuleta pamoja watu wa asili mbalimbali Afrika Kusini.
Mwandishi wa BBC Karen Allen aliye nchini humo anasema amekutana na mmoja wa walioshiriki maandamano dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi 1976.
Anasema maandamano hayo ni kama “mwanzo wa jambo”.
Amesema hiyo ni mara yake ya kwanza kushiriki maandamano tangu wakati huo.
Bintiye mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nodel Askofu Desmond Tutu naye amejiunga na wanaomtaka Rais Jacob Zuma ang’atuke.
Amenukuliwa na tovuti ya habari la DispatchLive akisema: "Huwa twawachagua viongozi wetu na tunaweza kuwang’atua.”
Mpho Tutu ameambia mkutano mkubwa wa #ZumaMustFall mjini Cape Town kwamba wanataka ufisadi nchini humo ukomeshwe.
Wakosoaji wa Rais Zuma wanasema ufisadi umezidi chini ya utawala wake.
Amekanusha vikali madai hayo.
Leo Bw Zuma, akiongoza sherehe za kuadhimisha Siku ya Maridhiano, ameahidi kukabiliana na ukosefu wa usawa miongoni mwa watu wa asili mbalimbali.
Hakuzungumzia maandamano dhidi yake.

posted by nick j

Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza.
Rais wa Burundi Piere Nkuruzinza

 BUJUMBURA.

Serikali ya Burundi inadai kwamba washambuliaji 12 wamefariki dunia na watu wengine 21 kutekwa nyara, huku upande wa askari jeshi wa serikali watano  wamejeruhiwa katika mapigano makali kuwahi kutokea tangu nchi hiyo ilipotumbukia katika mgogoro wa kisiasa mwezi April mwaka 2015.
Milio ya bunduki na milipuko imesikika alfajiri ya Ijumaa baada ya watu wenye bunduki kushambulia vituo viwili vya jeshi. Msemaji wa rais Willy Nyamitwe ameandika kwenye ukurasa wa tweeter kuwa mashambulio yalifanywa kwa lengo la kujaribu kuwaachia huru wafungwa waliokuwa kwenye kambi hizo za kijeshi.
Moja ya kambi iliyoshambuliwa ni ile la Ngagara, kaskazini mwa Bujumbura, lakini hakuna habari kamili zinazojulikana kuhusu tukio hilo.
Magari ya polisi na ya kijeshi yanashika doria katika mji wa Bujumbura huku kukiwa na raia wachache waliotoka nje.
Burundi imetumbukia katika mzozo wa kisiasa tangu mwezi April wakati Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwa atagombania mhula wa tatu na hatimaye kushinda katika uchaguzi.
Umoja wa Mataifa unaeleza kwamba tangu kuanza kwa ghasia hizo takriban watu 240 wameuliwa na laki mbili kukimbia makazi yao na kwenda nchi za jirani.
Wakati huo huo mashirika ya ndege ya Kenya Airways na Rwanda Air yametangaza kusitisha safari zake kuelekea mji mkuu wa Bujumbura kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama katika mji mkuu huo.
               

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget