Halloween Costume ideas 2015
Articles by "SIASA"

 

Kwa mara ya kwanza tangu Kamati Kuu ya CCM ilipomuengua kwenye kinyang’anyiro cha uspika, Samuel Sita ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa, jana ameweka bayana mustakabali wake; ameamua kustaafu siasa.

Sitta aliongoza kwa mafanikio Bunge la Tisa kiasi cha kumfanya apewe kirahisi uenyekiti wa Bunge la Katiba na hivyo kujijengea jina miongoni mwa wana-CCM kiasi cha kujitumbukiza kwenye mbio za urais na baadaye kutaka kurudi tena kuliongoza Bunge la Kumi na Moja.

Lakini hakufanikiwa kupitishwa kuwania urais wala kugombea uspika, ambao aliahidi kuwa angeengulkiwa angefika hata mahakamani.
Lakini jana alikuwa na kauli tofauti.

“Mambo ya siasa kwa sasa basi,” alisema Sitta alipoulizwa na kuhusu mipango yake ya baadaye baada ya kutopitishwa na CCM kuwania uspika.

Sitta ambaye amewahi kuongoza wizara mbalimbali, alisema kwa sasa anajikita katika uandishi wa vitabu na kwamba kwa umri alionao na utumishi wake serikalini, umefika wakati kwake kupumzika na kutoa ushauri wa masuala mbalimbali kwa wale watakaohitaji mchango wake.

Novemba 15, Kamati Kuu ya CCM ilimtosa Sitta na wengine waliojitokeza kuwania uspika na badala yake ikateua majina matatu kwa ajili ya kupigiwa kura na wabunge wa CCM, ambao walimchagua mbunge wa Kongwa, Job Ndugai kuwa Spika.

Kuenguliwa kwa Sitta kulikuwa ni pigo lake la pili katika nafasi ya hiyo baada ya kukatwa na kikao hicho mwaka 2010 alipokuwa akitetea nafasi yake. Wakati huo Anne Makinda alichaguliwa kuongoza Bunge la Kumi lililomaliza muda wake mwaka huu.

Sitta alijizolea sifa wakati akiwa Spika wa Bunge la Tisa kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, baada ya kuliongoza kuibua mijadala mbalimbali dhidi ya Serikali na kashfa ya Richmond iliyomfanya Edward Lowasa kujiuzulu uwaziri mkuu.

Baada ya kung’atuka
Alipoulizwa atajishughulisha na nini baada ya kustaafu, Sitta ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba alisema: “Nipo tu nyumbani nimepumzika. Naridhika na niliyoyafanya kwa Taifa. Wale watakaotaka kupata ushauri wakinifuata nitawasikiliza.”

Alisema kwa sasa anaandika makala ambazo baadaye ataziweka katika kitabu chake kitakachoeleza hali ya nchi na historia za masuala mbalimbali.

“Ninachokiandika ni mtazamo wangu binafsi, ni jinsi ambavyo mimi ninaona kwa macho yangu,” alisema.

Alipoulizwa kama atakubali kuongoza wizara iwapo Rais John Magufuli atamteua kuwa mbunge na kisha waziri alisema: “Tusizungumze jambo ambalo halina mwelekeo huo.”

Hata hivyo, alisema kwa mtazamo wake hadhani kama anaweza kufikiriwa kuwamo katika baraza hilo.

Kupinga uspika kortini

Kuhusu sakata la uspika, Sitta alisema angekwenda mahakamani kupinga kuondolewa kwake, kama tu mchakato wa chama hicho ungefanyika bila kufuata taratibu na watu kuonewa.

Katika mazungumzo yake na Radio Uhuru FM wakati wa mchakato wa uspika, Sitta alisema kutokana na hali ya joto la kisiasa ilivyo, ambayo ilidhihirika zaidi wakati wa uchaguzi, wabunge walioshinda ni vijana na ni wazi spika anayehitajika ni mwenye uzoefu.

Alisema licha ya kwamba wapo waliojaribu kumshawishi asigombee nafasi hiyo tena, badala yake awe anatoa ushauri pale inapobidi, alisisitiza bado ana wito wa kuwatumikia wananchi kwa njia hiyo.

“Niliposema (nitakwenda mahakamani) kama nisipoteuliwa na CCM kuwania uspika nililenga kama kitatokea kitu kama uonevu. Yaani kama vingeletwa vigezo ambavyo havipo katika mchakato,” alisema.

“Kama unakumbuka mwaka 2010 kililetwa kigezo cha ‘spika mwanamke’. Hicho ndicho kitu ambacho nilikilenga kwamba kikijitokeza sitakikubali. Uzuri ni kuwa hakikuwapo na kumbuka kuwa jambo lile (la kupitishwa kuwania uspika) lilikuwa ni uamuzi wa chama si mtu,” alisema Sitta.


Mwanamuziki Bebe Cool Mwenye Tisheti ya njaro akitumbuiza kabla ya Mkutano kuanza huko Bugiri. (Picha na Ofwono David)


Huku kampeni za Siasa zikizidi kuchanja mbuga nchini Uganda tayari wanamuziki wa nchi hiyo wameanza kujitokeza na kuungana na wagombea Urais katika kuhamasisha katika Mikutano yao. Leo Msanii wa Muziki wa mwenye heshima nchini humo Bebe Cool aliburudisha wananchi wa Uganda katika Mkutano wa Siasa wa Yoweri Museveni.

Tazama picha Kadhaa za Bebe Cool akitumbuiza katika Mkutano kabla ya Mgombea Urais Kupitia chama cha NRM kuwasili Mkutanoni. 

 

 

 


(Picha zote na Ofwono David)

Mgombea urais Kwa Tiketi ya NRM nchini Uganda Ndugu Yoweri Museven Akiwasili mkutanoni. (Picha na Ofwono David)


Ikiwa Duru la siasa nchini Uganda likizidi kupamba moto huku zikiwa zimekwisha katika takribani siku arobaini na moja tokea pale kipyenga cha kampeni za kunadi sera za wagombea kwa wananchi kilipopulizwa mnamo novemba 9.

Mchuano mkali umeonekana kati ya Mgombea nafasi wa Urais kupitia chama cha NRM anayetetea kiti chake Ndugu Yoweri Kaguta Museveni dhidi ya Mpinzani wake Mkubwa Kupitia chama cha FCD Party Ndugu Kiiza Besigye.

Hata hivyo leo Mgombea kiticho cha urais kwa tiketi ya NRM Ndugu Museveni Amefanya Mkutano wa Kampeni katika kaunti ya Busiki iliyopo wilayani Namutumbu.




Ndugu Yoweri Kagutu Museveni Akizungumza na wananchi wa Kaunti ya Busiki wilayani Namutumba. (Picha na Ofwono David)

Maelfu ya wananchi wa Kaunti ya Busiki wakiwa katika Mkutanoni. (Picha na Ofwono David)




 


MGOGORO ZANZIBAR
 
Mosi, Mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu atangazwe haraka ili hali ya utulivu wa kawaida irejee. Mshindi ale kiapo, aunde Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuwaunganisha Wazanzibari.
Pili, ACT-Wazalendo imebaini kuwapo kwa idadi kubwa isivyo kawaida ya wanajeshi wanaolinda Bandari, Uwanja wa Ndege, Vituo vya Redio na maeneo mengine muhimu. Chama chetu kinataka askari hao warejee makambini kwao kwani uwepo wao katika maeneo ya kiraia unasababisha hali ya shaka na hofu miongoni mwa wananchi.

Tatu, kwa ajili ya mustakabali mwema wa Zanzibar, ACT-Wazalendo kinataka mazungumzo yoyote kuhusu uchaguzi uliofutwa yahusishe wadau wa vyama vyote na taasisi nyingine walioshiriki kwenye uchaguzi.
Hii si mara ya kwanza kwa viongozi wa vyama vya CCM na CUF kukutana na kufanya mazungumzo baada ya kutokea matatizo. Lakini uzoefu unaonyesha kwamba suluhisho huwa si la kudumu na badala yake matatizo yaleyale hujirudia baada ya muda.

Suluhisho la hali hii ni vyama vingine vyote, kujumuishwa katika aina hii ya mazungumzo ili kupata mawazo jumuishi na yatakayowakilisha sehemu kubwa zaidi ya Wazanzibari ambao wengi wao, hasa kizazi kipya, hawana uhusiano wowote na vyama hivyo viwili.

Kwa ujumla hali ya kisiasa Zanzibar ni mbaya sana na inatisha kwani wananchi wanaishi kwa hofu kubwa na hawaelewi kinachoendelea, ukimya uliotamalaki hauashirii hatima njema ya siasa za Zanzibar.
ACT-Wazalendo kinapenda kutumia nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa subira na uvumilivu wa kiwango cha juu waliouonyesha katika kipindi hiki cha hali ya sintofahamu.

Imetolewa leo, Desemba 20, 2015.
Mji Mkongwe, Zanzibar

Kabwe Z Ruyagwa Zitto, Mb
Kiongozi wa Chama


Waaasi Thomas Lubanga na Germain Katanga


Makama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC,imewarejesha nchini Demokrasia ya Congo, waasi wawili, Thomas Lubanga na Gemain Katanga ili waweze kutumikia vifungo vyao nchini humo.
Lubanga alishtakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita,ICC kutokana na makosa ya kuwa ajiri watoto wadogo katika kundi lake la waasi na kusababisha mauaji na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kati ya mwaka 2002 na 2003.

Germain Katanga yeye anayedaiwa kuongoza kundi lililofanya mauaji ya zaidi ya watu 2000, katika wilaya ya Ituri Mashariki mwa demokrasia ya Congo.
Waasi hawa watamalizia vifungo vyao jijini Kinshasa Demokrasia ya Congo.


Waziri mkuu wa zamani wa Uganda  Amama Mbabazi,akizungumza na waandishi wa habari katika mji wa Jinja masjhariki mwa  Uganda, Sept. 10, 2015.
Waziri mkuu wa zamani wa Uganda Amama Mbabazi,akizungumza na waandishi wa habari katika mji wa Jinja masjhariki mwa Uganda,




Kampeni za uchaguzi zikipamba moto huko Uganda kumekuwepo na ripoti za mapambano kati ya wafuasi wa serikali na Upinzani katika maeneo mbali mbali ya nchi.
Mapambano kati ya wafuasi wa Yoweri Museveni na waziri mkuu wa zamani Amama Mbabazi yametokea huko Kaskazini ambako ndio ngome ya rais baada ya vijana waliovalia fulana zenye picha za  rais Museveni kuvamia mkutano na kuanza fujo.


Watu tisa wamejeruhiwa katika sakata hilo na wawili kati yao wakiwa katika wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali ya Ntungamo magharibi mwa Uganda baada ya vijana hao kuwashambulia wenzao kwa ngumi na mateke na fimbo.
 
Kwa mujibu wa Amama Mbabazi  fujo hizo zimekuwa zikifanyika mara kadhaa na ameomba msaada tume ya uchaguzi lakini hajasaidiwa akisema kwamba huu ni ushindani tu, sio suala la kufa na kupona.
Msemaji wa Polisi Fred Enanga amesema uchunguzi unaendelea kuhusu mkasa huo na hivi sasa wanashikilia washukiwa wawili.

Kwingineko polisi wamefyatua risasi hewani kuwatawanya vijana wanaomuunga mkono mgombea wa urais kupitia chama cha FDC Dkt. Kiiza Besigye, waliokuwa wanataka kumchoma kijana anayedaiwa kuwa mfuasi wa chama cha NRM aliyejaribu kuingilia  mkutano wake Besigye.
 

  

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget