Halloween Costume ideas 2015
Articles by "BURUDANI"

Bondia wa zamani mbabe aliyeweka rekodi za nguvu kwenye mchezo wa ngumi, Mike Tyson ameamua tu kutuonesha kwamba kama huwezi kutembelea hoverboard, basi wewe achana nazo tuu hata usijaribu kucheza nazo.
Hii video aliipost Mike Tyson kwenye ukurasa wake Instagram ambapo kuna sauti ya mtoto wa kike inaonekana kama anamuonya hivi kwamba ataanguka, lakini Mike akaendelea zake.. sekunde chache mbele mambo yakaenda kombo !!
Ilikuwa stori yenye uzito wake kiasi cha kwamba TV ya CNN waliiripoti hii.

Staa wa R&B wa Marekani Chris Brown amekuwa haishiwi headlines..baada ya matukio mfululizo yakimuhusisha na Polisi, headlines zimerudi tena kwake.
Ukiachia lile tukio la kumpiga mwanamuziki mwenzake Rihanna mwaka 2009 na kutakiwa kutojihusisha na kosa lolote kwa miaka mitano hili ni tukio lingine lilolomrudisha kwenye mikono ya polisi huko Las Vegas.
Jana jumamosi akiwa katika klabu ya The Palms Casino Resort staa huyo anadaiwa kumpiga usoni mama mmoja Liziane Gutierrez ambaye alikua akijaribu kumpiga picha.
Liziane Gutierrez
Polisi katika jiji la Las Vegas, Marekani bado wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na malalamiko ya mama huyo
Mwaka 2009, Brown aliagizwa kukaa miaka mitano bila kufanya kosa baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga nyota wa muziki wa pop Rihanna.

Rapa Lil Wayne ametajwa kuongoza orodha ya wasanii wanaotumia maneno machafu zaidi kwenye nyimbo zao “foul-mouthed artist”.
Digital music streaming service Deezer imemtaja rapa Lil  Wayne baada ya kuangali na kusikiliza nyimbo milioni 35 walizonazo kwenye system yao. Lil Wayne ana nyimbo mbili kwenye nyimbo 10 zenye matusi zaidi duniani.
Wimbo wake wa ‘Beat the S**t’ unamatusi 188 akifuatiwa na rapa Snoop Dogg.
Hii ndio orodha ya Deezer ya wasanii kumi wenye nyimbo zenye maneno machafu zaidi.
  1. Lil Wayne
  2. Snoop Dogg
  3. Jay Z
  4. 2Pac
  5. DMX
  6. Eminem
  7. Rick Ross
  8. Busta Rhymes
  9. 50 Cent
  10. Ice Cube
Album zenye matusi mengi zaidi duniani.
Mickey Avalon, Mickey Avalon – 3,094 curse words
All Eyez on Me (Dual Disc), 2Pac – 1,091 curse words
Until the End of Time, 2Pac – 800 curse words
Turn Up Why Turn Down, DJ Dallas Green – 779 curse words
All Eyes on Me, 2Pac – 752 curse words
R U Still Down? (Remember Me), 2Pac – 740 curse words
I Am Not a Human Being (Deluxe Edition), Lil Wayne – 722 curse words
Still Smokin and Leaned Out, Lil Wayne – 700 curse words
Anarchy, Busta Rhymes – 677 curse words
Blood Moon: Year of the Wolf, Game – 675 words

Kabla hajawa dj mkubwa Marekani na Duniani, Dj Khaled aliweza kuwapa nafasi ya kung’ara wasanii wakubwa kama Birdman,Lil Wayne na Mavado kwa kusambaza na kutangaza kazi zao mitaani.
Wazazi wa Dj Khaled walikuwa wasanii na walipendakufanya muziki wa kiarabu.
Khaled alikuwa na duka la muziki mjini New Orleans na mwaka 1993 alikutana na Birdman na Lil Wayne.
Khaled aliendelea na harakati za muziki mpaka kuja kuwa mtangazaji wa kipindi cha The Luke Show. Mwaka 2003 Khaled alianzisha kipindi chake cha radio WEDR.
Baada ya kuwa karibu na wasanii kwa muda mrefu Dj Khaled aliona ni nafasi nzuri kuwatumia wasanii hawa kutengeneza pesa ambazo zitawafaidisha wote na mwaka 2006 kuelekea 2008 Khaled aliwakutanisha wasanii wakubwa kwa mara ya kwanza na kutengeneza album ya Listennn… the Album and We the Best.

Utathmini wa takwimu kuhusu watoto wanaozaliwa Uingereza umebaini mimba nyingi hutungwa wakati wa Krismasi kuliko wakati mwingine wowote ule wa mwaka.
Takwimu hizo za kipindi cha miongo miwili kutoka Idara ya Taifa ya Takwimu zinaongeza watoto wanaozaliwa huongezeka sana wiki 40 (miezi 9) baada ya msimu wa sikukuu.
Hili huenda linatokana na wanandoa kutumia muda mwingi pamoja wakisherehekea, au kulenga makusudi mwanzo wa mwaka mpya wa shule ambao huanza mapema Septemba nchini humo.
“Ongezeko la watoto wanaozaliwa mwishoni mwa Septemba ni ishara kwamba mimba nyingi hutungwa wiki chache kabla ya Krismasi na kuendelea hadi siku chache baada Krismasi kuliko wakati mwingine wowote wa mwaka,” idara hiyo imesema.
Kawaida watoto 1,800 huzaliwa kila siku lakini idadi hii hupanda hadi 1,974 siku yenye kuzaliwa watoto wengi zaidi ambayo ni Septemba 26.
Siku zinazoshuhudia idadi ndogo zaidi ya watoto wanaozaliwa ni siku za Krismasi, Boxing Dei na siku ya Mwaka Mpya.
Hili sana huenda linatokana na idadi ndogo ya watu wanaopangiwa kujifungua kwa kufanyiwa upasuaji siku hizo, kwani huwa ni siku za mapumziko.
Profesa wa masuala ya uzazi kutoka Chuo Kikuu cha Sheffield Allan Pacey ameambia BBC: “Wazo kwamba mimba nyingi hutungwa wakati wa Krismasi lina msingi. Nina uhakika sherehe na shamra shamra za wakati huu huchangia.”

posted by nickson john (NICK J)


Msanii na mwanamitindo Jack Patrick.
Na Brighton Masalu
JACK Patrick, msanii, mwanamitindo na mmoja wa Watanzania wanaotumikia kifungo nchini China kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya, ametoa kilio upya akiwa gerezani, baada ya kuwashutumu marafiki zake kushindwa kumtembelea, licha ya kufika mara kwa mara katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa barani Asia.
Kikizungumza na gazeti hili juzikati, chanzo kilichoomba hifadhi ya jina lake, ambacho kilimtembelea Jack katika gereza lililo mji wa Maccau, kilisema msanii huyo licha ya kuumizwa na mambo mengi, lakini usaliti unaofanywa na marafiki zake wa karibu ndiyo unamuuma zaidi.
“Jack alitarajia watu wake wa karibu aliokula nao bata wakati wa furaha wangeenda kumtembelea mara kwa mara akiwa gerezani, lakini badala yake imekuwa kinyume licha ya kuishi kama ndugu kipindi cha nyuma.
“Badala yake wanaomtembelea ni watu ambao hakuwahi kuwa nao karibu kabla, hili linamuuma sana na ameahidi akitoka atajitafakari upya urafiki wake na watu hao,” kilisema chanzo chetu kikimnukuu msichana huyo aliyehukumiwa mwaka 2013 kwenda jela miaka sita.

posted by nick j 

 Agnes Masogange.
MWANAMITINDO Agnes Masogange, amekana kuwa na ujauzito wa mwanamuziki maarufu wa Nigeria aitwaye Davido, hii ni baada ya Agnes kuandika kwenye mtandao kuonyesha upendo wake kwa mwanamuziki huyo.
Hata hivyo, Agnes amemaliza mkanganyiko huo na kuzifuta picha zote zilizoleta taharuki na kuweka picha ya mpenzi wake halisi wa kiume.
Hata hivyo, Davido bado hajatoa kauli yoyote kuhusu suala hilo.

 Bondia maarufu duniani, Floyd Mayweather yupo mapumzikoni dubai.
 Kama sehemu yake ya matumizi ya kawaida bondia huyo ameamua kuonyesha jeuri nyingine ya fedha baada ya kununua saa ya mkononi yenye thamani ya dola milioni 1 sawa na fedha za kitanzania zaidi ya milioni 200.
 Saa hiyo aina ya Hublot ndio saa ghali zaidi duniani kwa sasa.
Myweather akiwa katika jengo maarufu duniani la Burj Khalifa ambapo ndipo alipofikia.

posted by nick j von luvendowski

Rapa Drake ametajwa kuwania tuzo tano za Grammy mwaka huu kupitia nyimbo zake “Back to Back” na Best Rap Song for “Energy”ila lebel yake ya Cash Money ingeweza kuongeza namba ya tuzo anazowania mwaka huu.
Wimbo mmoja ambao watu wameshanga haujatajwa kwenye tuzo hizi ni wimbo wa “Hotline Bling,” wenye mafanikio kuliko “Back To Back” na “Energy” .
Hits Daily Double imetoa repoti kuwa lebel ya Cash Money haikupeleka wimbo huo kwenye tuzo hizo. Wimbo huu ungekuwepo kuna uwezekano ungeshinda “Record of the Year.”
Drake alishinda tuzo ya Grammy kwenye kipengele cha Best Rap Album mwaka 2012 kupitia album ya Take Care.

Nahreel ni msanii wa kundi la Navy Kenzo lakini pia ni Producer ambaye mikono yake imehusika kuzisuka hits nyingi tu ikiwemo za WEUSI, Vanessa Mdee, Navy Kenzo, Shilole na hivi karibuni Nahreel ameingia kwenye headlines za Tanzania baada ya kusema hakupendezwa na maneno ya utambulisho wake kufutwa kwenye beat aliyoitengeneza ya wimbo wa ‘Nana‘ wa Diamond Platnumz ft. Mr Flavour
Nahreel anasema alikiweka hicho kibwagizo kikimtaja kwamba yeye ndio producer wa hiyo beat lakini wimbo ulipotoka hakukisikia sababu kiliondolewa, ikabidi aulize upande wa Diamond imekuaje…. kumsikia mwenyewe na alichoambiwa unaweza kubonyeza play kwenye hii video hapa chini. 
POSTED BY Nick J Von Luvendowski

Alex Kassuwi akimpokea Mario Hugh Knignt Jr. aka Suge Knight bara baada ya kuwasili Bongo.
Mwaka 2013 Kampuni ya Africa Swahili Media ilifunguliwa Rasmi na kuanza kuwekwa mikakati sahihoi ya kuhakikisha inafanya vizuri katika soko la habari. Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa The CEO wa Kampuni ya Africa Swahili Media Mr. Davis Mosha alimtembelea Suge Knight  ambaye ni Muwekezaji na Mjasiriamali mkubwa na pia alikuwa CEO wa Black Capital Records na pia amewahi kuwa CEO wa Death Row Records. Suge Knight amewapa mafanikio makubwa wanamuziki mbalimbali kama Tupac Shakur, Dr. Dre, Snoop Dogg Dogg,Outlaws na Tha Dogg. 


CEO wa Africa Swahili Media Mr Davis Mosha akiwa na Suge Knight huku akiwa ameambatana na Mtoto wake Edger Mosha.

Suge Knight aliwasili Hotel aliyofikia CEO wa Africa Swahili Media iliyopo Marriott LA nchini Marekani. kwa Ujio wa kufanya mazungumzo na CEO wa Africa Swahili Media Mr. Davis Mosha na kukubaliana kuanza kuitangaza kampuni hiyo ambayo pia ipo nchini Marekani. Africa Swahili Media ni kampuni yenye lengo la kuwa na vyombo vya habari ambavyo vitakuwa vikisambaza habari za Africa katika bara lote la Africa na Duniani kote. Kwa sasa Kampuni hiyo inafanya matengenezo ya Studio zake za kisasa za Radio na Tv ambavyo vitaanza kusikika hivi karibuni. 

Hii ndiyo Crew ambayo Suge Knight aliongozana nayo alipoenda kuzungumza na Mr. Davis Mosha


XXL ya cloudsFM kila mwaka hufanya party ya wanafunzi wote waliofunga shule ikiwa ni pamoja na wa shule ya Msingi,Sekondari,kwa pamoja party hii inaitwa After skul Bash,hii inaendelea sasa hivi katika ufukwe wa bahari  Escape 1 Mikocheni Dar es Salaam.
Wasanii waliotoa burudani katika jukwaa akiwemo Joh Makini,M Rap, G Nako, Nahreel, Aika, Jux, Ruby,Stereo, Makomando na wengineo.







MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget