Halloween Costume ideas 2015
Articles by "KIMATAIFA"

Saudi Arabia imesitisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi ya Iran na huku kukiwa na hali mbaya ya mvutano kufuatia utekelezaji adhabu ya kifo kwa mhubiri maarufu wa dini ya Kiislamu.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Saudia, Adel al-Jubeir, ameishutumu serikali ya Iran kwa kusambaza silaha na kuanzisha jela na kuwafunga watu wanaodhaniwa magaidi katika ukanda wake .
Waziri huyo amesema wanadiplomasia wa Iran wanatakiwa kuondoka Saudia ndani ya saa arobaini.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, waandamanaji mjini Tehran waliuvamia ubalozi wa Saudia mjini Tehran, huku wakilaani utekelezaji wa hukumu ya kifo kwa Sheikh Nimr al-Nimr na watu wengine 46.
Watu hao waliouawa inasadikiwa walikuwa na hatia ya makosa yanayohusiana na ugaidi.
Kiongozi mkuu wa Iran alimweleza Sheikh huyo kama shahidi ambaye alikuwa akitetea amani na kufanya maandamano ya amani.

NICKSON JOHN







 ARGENTINA
                                                                                                                                          

Mkuu wa huduma ya magereza katika mji Buenos Aires Argentina amefutwa kazi baada ya wafungwa watatu mashuhuri walioshikiliwa gerezani hapo kwa  makosa ya mauaji kutoroka kutoka gereza lenye ulinzi mkali siku ya Jumapili....,

 



Gavana wa jimbo hilo , Bi Maria Eugenia Vidal , alisema yeye alichukua hatua hiyo kwa sababu kulikuwa na ushahidi kwamba wafungwa wote walisaidiwa na maofisa wa idara ya magereza kukamilisha mpango wao wa kutoroka .

 

 Wafungwa hao Victor Schillaci na kaka wawili Cristian na Martin Lanatta, walikuwa wanatumikia hukumu ya maisha gerezani kwa makosa ya utekaji nyara na mauaji ya wafanyabiashara watatu katika tukio lililohusishwa na mzozo wa madawa ya kulevya mnamo mwaka wa 2008.

Wafungwa hao walitoroka kutoka kwenye gereza lenye ulinzi mkali huku wakitumia bunduki bandia kutishia mmoja wa walinzi wa gereza hilo.
…………………………………………………….



Wanachama wa National Front of Liberation Agaton Rwasa na Leonce Ngendawmana katika mazungumzo ya amani.


Wanachama wa National Front of Liberation Agaton Rwasa na Leonce Ngendawmana katika mazungumzo ya amani.



UGANDA
                                                                                                                                               

Mazungumzo ya Burundi ambayo yameanza rasmi jana huko Kampala Uganda yanaelekea kukutana na vikwazo hasa baada ya serikali ya Burundi kutoa taarifa na kukosoa vikali maandalizi ya kikao hicho.....,

 




 Mchambuzi wa siasa za Uganda Akol Amazima anasema "Serikali ya Burundi imeingia kwenye mazungumzo hayo na mtazamo hasi na duru za kisiasa nchini humo zinaitaka jamii ya kimataifa isilegeze kamba juu ya mzozo huo".


Mazungumzo hayo yako chini ya upatanishi wa rais Yoweri Kaguta Museveni. Serikali ya Burundi kupitia taarifa iliyosaniwa na mkuu wa ujumbe wa serikali katika kikao cha Jumatatu  jijini Entebe waziri wa mambo ya nje Alain Nyamitwe inalaani kile walichosema mpatanishi alialika makundi ambayo hayatambuliwi na sheria za Burundi.

Kundi hilo ni muungano wa wanasiasa wa upinzani na wanaharakati wa kiraia wanaodai kutetea hadhi ya makubaliano ya Arusha ambao walitoroka nchi baada ya kudhihirisha upinzani wao dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza.

Vile vile serikali ya Burundi inasema kuwa hawakubaliani juu ya muendelezo wa mazungumzo hayo ambapo baada ya uzinduzi jijini Uganda vikao vitaendelea jijini Arusha Tanzania tarehe 6 januari.

                                           




Wachuzi wakifanya biashara zao mjini Harare, Zimbabwe
Wachuuzi nchini Zimbabwe wakisubiri wateja wa nguo.


 ZIMBABWE
                                                                                                                    

Uchumi wa Zimbabwe unamalizika mwaka huu ukibashiriwa kuwa bei zitaendelea kushuka mwakani. Lakini wachumi wanasema mwenendo huo huenda usimnufaishe mtu yeyote.





Wazimbabwe wengi wanaonekana kuwa katika hali mbaya zaidi leo kuliko hapo mwaka 2009, pale taifa hilo la kusini mwa Afrika lilipoachia sarafu yake  isiyo na thamani  na kuanza kutumia sarafu mbali mbali  hususan dola ya marekani. Baada ya miaka ya mfumuko mkubwa wa bei, bei sasa zimetulia na mambo yanaonekana kubadili mwendo. Sasa kuna kushuka kwa bei nchini Zimbabwe.
Lakini John Robertson,mchumi huru  hapo mjini Harare anaeleza kuwa hizo si habari njema, kwa wazimbabwe wala  kwa serikali ya rais Robert Mugabe.

Robertson anasema, kushuka kwa bei kwa kawaida kunahusishwa  na watu kuwa na fedha za kutumia, lakini kuchaguwa kutonunuwa kile wanachokitaka kwa sababu kitakuwa rahisi zaidi mwezi ujao au baada ya miezi miwili au mitatu. Kile kilichokuwa kikipunguka nchini Zimbabwe ni rai ya ununuzi. Mishahara ya serikali inalipwa kutokana na pato la kodi ya serikali na pato hilo linashuka. Kwa hiyo serikali haina uwelewa wa maendeleo kwenye masoko.

Robertson anasema kutokana na mapato  na hali ya kiuchumi, serikali inapaswa kupunguza shughuli zake. Kwa vile haijafanya hivyo, Robertson anasema hilo linaeleza kwa nini serikali ya Mugabe haiwezi kuwalipa wafanyakazi wake mishahara mwezi huu. Pato linapunguka, lakini idadi ya wafanyakazi inaongezeka. Wafanyakazi wa serikali wanatumia Zaidi ya asli mia 85 ya pato yanayokusanywa.

Gift Mugano, mdhahiri mwandamizi  wa uchumi katika chuo kikuu cha Zimbabwe, na ni mshauri wa serikali. Anaelezea safari ya Zimbabwe ya mfumuko mkubwa wa bei na kushuka kwa bei. Anasema hali zote za kiuchumi zimesababisha mashaka kwa wazimbabwe wengi. Sehemu ya tatizo ni udhaifu wa Rand ya Afrika kusini na Kwacha ya Zambia, ambazo zimepelekea kupunguzwa kwa bei za bidhaa Zimbabwe inazonunua kutoka nchi hizo mbili.

Kwa hiyo huko nchini Zimababwe,  kulikuwa hakuna  bidhaa za kununuliwa mwaka 2009, hivi sasa hakuna fedha za kununuwa bidhaa zilizopo pale mwaka 2015 unapomalizika. Wote Mugano na Robertson wanasema kuna haja ya kubuni uwekezaji ili kuwa na  wigo mpana wa mapato  na ajira nchini Zimbabwe ili kushughulikia suala la kushuka kwa bei.
                                                                                                         


Waziri wa haki wa Afrika Kusini amefutilia mbali ombi la kutaka kesi inayomkabili mfalme wa jamii ya Nelson Mandela ya Thembu isikizwe upya.




AFRIKA KUSINI
                                            

Waziri wa haki wa Afrika Kusini amefutilia mbali ombi la kutaka kesi inayomkabili mfalme wa jamii ya Nelson Mandela ya Thembu isikizwe upya.






Mfalme huyo , Buyelekhaya Dalindyebo alipatikana na hatia ya kushambulia watu , uteketezaji wa mali na kuhujumu mkondo wa sheria.
Makosa yake yanahusishwa na dhulma dhidi ya raia aliokuwa akitawala miaka ya 90, kwenye shamba alilomiliki mashariki mwa mji wa Cape.

Mfalme huyo aliteketeza nyumba za wapangaji watatu, akitaka kuwafukuza, kwa madai kuwa walikiuka sheria za jamii yao. Pia, alishambulia watu watatu hadharani kwa madai ya uhalifu.

Mahakama nchini Afrika ya kusini ilimhukumu kifungo cha miaka 12 gerezani.
Badala ya kujikibadhi kwa mamlaka, mfalme huyo wa aba Thembu, aliwasilisha ombi kwa mahakama, akisema kuwa hakuhukumiwa kwa haki.
Hata hivyo ombi lake limekataliwa hii leo jumanne, na waziri wa mahakama Michael Masutha, kwani hakutoa ushahidi mpya.
Mfalme huyo amesema kuwa hatokubali uamuzi huo, na anataka muda wa dhamana yake uongezewe.
                                                                                                                 

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget