Halloween Costume ideas 2015
Articles by "HABARI"

Chuo kikuu cha Garissa kilichofungwa mwaka uliopita baada ya watu 148 kuuawa kwenye shambulio lililotekelezwa na wanamgambo wa al-Shabab, kimefunguliwa tena.
Wafanyakazi wamefika kazini leo huku usalama ukiwa umeimarishwa.
Kila aliyekuwa akiingia katika chuo kikuu hicho kilichoko eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya amepekuliwa na maafisa wa usalama.
Kituo cha polisi, ambacho kitakuwa na maafisa zaidi ya 20 wa kutoa ulinzi, kimejengwa ndani ya chuo kikuu hicho.
Kitambulisha mada #GarissaUniversityReopens (Chuo Kikuu cha Garissa chafunguliwa tena) kimekuwa kikivuma katika mtandao wa Twitter nchini Kenya.
Wengi wanasema kufunguliwa kwa chuo hicho kunaonyesha Wakenya hawawezi kuvunjwa moyo na magaidi.
Msimamizi mkuu wa chuo kikuu hicho Prof Ahmed Warfa ameambia BBC kwamba wanafunzi wataanza kufika chuoni Jumatatu ijayo tarehe 11 Januari.
Hakukukuwa na sherehe yoyote maalum ya kuadhimisha kufunguliwa upya kwa chuo hicho.
Wengi wa wanafunzi wanaofadhiliwa na serikali walionusurika shambulio hilo la mwezi Aprili walihamishiwa Chuo KIkuu cha Moi, Eldoret.
Wanafunzi wa kujitegemea ndio wanaotarajiwa kurejelea masomo Jumatatu.
Mwandishi wa BBC Bashkas Jugsodaay anasema kufunguliwa kwa chuo kukuu cha Garissa ni afueni kwa wakazi na viongozi wa mkoa wa Kaskazini Mashariki ambao wamekuwa wakiisihi serikali kufungua chuo hicho, kwa walikuwa wakikitegemea kwa ajira na wateja. Wengi walikuwa wakinufaika
Wanafunzi zaidi ya 800 walikuwa wakisomea taaluma mbalimbali katika chuo hicho kabla ya kushambuliwa na magaidi Aprili mwaka jana.

Saudi Arabia imesitisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi ya Iran na huku kukiwa na hali mbaya ya mvutano kufuatia utekelezaji adhabu ya kifo kwa mhubiri maarufu wa dini ya Kiislamu.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Saudia, Adel al-Jubeir, ameishutumu serikali ya Iran kwa kusambaza silaha na kuanzisha jela na kuwafunga watu wanaodhaniwa magaidi katika ukanda wake .
Waziri huyo amesema wanadiplomasia wa Iran wanatakiwa kuondoka Saudia ndani ya saa arobaini.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, waandamanaji mjini Tehran waliuvamia ubalozi wa Saudia mjini Tehran, huku wakilaani utekelezaji wa hukumu ya kifo kwa Sheikh Nimr al-Nimr na watu wengine 46.
Watu hao waliouawa inasadikiwa walikuwa na hatia ya makosa yanayohusiana na ugaidi.
Kiongozi mkuu wa Iran alimweleza Sheikh huyo kama shahidi ambaye alikuwa akitetea amani na kufanya maandamano ya amani.

NICKSON JOHN

Edward Lowassa ambaye alikua mgombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 kupitia tikect ya CHADEMA, ameziweka hizi picha zake tatu akichunga Ng’ombe kisha akaandika haya maneno hapa chini.
>> ‘Ndugu zangu,naendelea kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Nikiwa shambani kwangu Mzeri, Handeni nikichunga mifugo yangu naona miujiza ya Mungu ikitendeka. Mazingira ya asili ni zawadi kuu aliyotukirimu Mwenyenzi Mungu. Kila mmoja wetu kwa nafasi yake amshukuru Mungu kwa kuyathamini, kuyalinda na kuyatunza mazingira popote alipo

BY NICKSON JOHN

Mzoga wa nyangumi umepatikana ufukweni nje ya mji Capetown Afrika Kusini.
Mzoga huo unaaminika kusombwa na maji ya bahari na kukwama kwenye mwamba.
Haijabainika kilichosababisha kifo cha nyangumi huyo.
Mwanidhi wa Swahili Media aliyeko huko Pumza Fihlani anasema kuwa maafisa wa afya wa umma wametangaza kuwa ufukwe huo utafungwa kwa umma leo, ilikufanikisha shughuli ya kuondoa mzoga huo uliowavutia halaiki ya watu mapema leo.

posted by nickson john (Nick J)

Rais wa Colombia , Juan Manuel Santos, ametia sahihi sheria mpya inayohalalisha matumizi ya bangi kwa manufaa ya kimatibabu
Katika hotuba kwa taifa kupitia kwa runing bwana Santos alisema kuwa sheria hii kimsingi inaiweka Colombia katika mtsari wa mbele wa kupamabana na matumizi ulanguzi na ukuzaji wa bangi Kusini mwa Marekani.
"Tumechukua hatua ya kwanza kuisadia Colombia kupambana na gonjwa hili sugu la matumizi ya mihadarati.
Sheria hii itasaidia kufaidi kile kinachoitwa kuwa uwezo wa kimatibabu ya mmea huu ;bangi.''alisema rais Manuel Santos.
Hata hivyo alisisitiza kuwa sheria hii mpya haikinzani hata kidogo na mswada wake wa kupambana na mihadarati.
" kufaidi uwezo wa utabibu wa bangi kwa hakika haizuii kwa vyovyote msimamo wetu dhabiti wa kupambana na matumizi ya mihadarati.''
Tutaendelea mbele na harakati za kupambana na ulanguzi wa madawa mengine haramu alisema rais Manuel Santos.
"Sheria hiyo mpya inaruhusu ukuzaji wa mmea huo kwa wale tu waliopewa idhini na serikali''
Colombia imekuwa mshiriki mkubwa wa serikali ya Marekani katika mikakati yake ya kupambana dhidi ya ulanguzi na ukuzaji wa mihadarati.
Taifa hilo limefaidi mabilioni ya dola katika misaada mbali na kutumia jeshi lake katika vita dhidi ya magenge ya walanguzi.
Santos alitangaza sheria hiyo mpya miezi michache tu baada yake kupiga marufuku upulizaji wa madawa ya Monsanto baada ya shirika la afya duniani WHO kusema kuwa utafiti umeonesha kuwa Roundup inasababisha saratani.

POSTED BY NICKSON JOHN (NICK J)

Utathmini wa takwimu kuhusu watoto wanaozaliwa Uingereza umebaini mimba nyingi hutungwa wakati wa Krismasi kuliko wakati mwingine wowote ule wa mwaka.
Takwimu hizo za kipindi cha miongo miwili kutoka Idara ya Taifa ya Takwimu zinaongeza watoto wanaozaliwa huongezeka sana wiki 40 (miezi 9) baada ya msimu wa sikukuu.
Hili huenda linatokana na wanandoa kutumia muda mwingi pamoja wakisherehekea, au kulenga makusudi mwanzo wa mwaka mpya wa shule ambao huanza mapema Septemba nchini humo.
“Ongezeko la watoto wanaozaliwa mwishoni mwa Septemba ni ishara kwamba mimba nyingi hutungwa wiki chache kabla ya Krismasi na kuendelea hadi siku chache baada Krismasi kuliko wakati mwingine wowote wa mwaka,” idara hiyo imesema.
Kawaida watoto 1,800 huzaliwa kila siku lakini idadi hii hupanda hadi 1,974 siku yenye kuzaliwa watoto wengi zaidi ambayo ni Septemba 26.
Siku zinazoshuhudia idadi ndogo zaidi ya watoto wanaozaliwa ni siku za Krismasi, Boxing Dei na siku ya Mwaka Mpya.
Hili sana huenda linatokana na idadi ndogo ya watu wanaopangiwa kujifungua kwa kufanyiwa upasuaji siku hizo, kwani huwa ni siku za mapumziko.
Profesa wa masuala ya uzazi kutoka Chuo Kikuu cha Sheffield Allan Pacey ameambia BBC: “Wazo kwamba mimba nyingi hutungwa wakati wa Krismasi lina msingi. Nina uhakika sherehe na shamra shamra za wakati huu huchangia.”

posted by nickson john (NICK J)

Mwanaanga Tim Peake, ambaye ndiye Mwingereza wa kwanza kwenda kituo cha kimataifa cha anga za juu, ameomba msamaha baada ya kupiga nambari ya simu isiyo sahihi kutoka anga za juu.
Mwanaanga huyo aliandika ujumbe wake wa kuomba msamaha kwenye Twitter baada ya kumpigia simu mwanamke na kusema: "Hello, is this planet Earth?" (Hujambo, hii ni sayari ya dunia?).
Bw Peake amesema kwenye Twitter kwamba simu hiyo haikuwa ya mzaha.
Hata hivyo, hakusema ni nani hasa aliyekuwa akimpigia simu.
Peake, baba wa watoto wawili anayetoka Chichester, Sussex Magharibi, alitua katika kituo cha kimataifa cha anga za juu (ISS) Jumanne 15 Desemba.
Atakaa katika kituo hicho miezi sita akifanya utafiti wa kisayansi.
Mapema wiki hii, aliwasaidia wanaanga wenzake wawili kutoka nje ya kituo hicho.
Wanaanga Tim Kopra na Scott Kelly, kutoka kituo cha Nasa cha Marekani walihitaji kutoka nje ya kituo hicho kukarabati kifaa kilichokuwa kimeharibika.

POSTED by Nickson John (NICK J)

Kiongozi wa kundi moja kuu la waasi nchini Syria ameuawa kwenye shambulio la angani katika viunga vya mji wa Damascus.
Zahroun Alloush, ambaye ndiye mwanzilishi wa kundi la Jaysh al-Islam ameuawa pamoja na viongozi wengine wa kundi hilo, ripoti zinasema. Walikuwa mkutanoni waliposhambuliwa kwa kombora, wanaharakati wamesema.
Kundi hilo la wapiganaji huungwa mkono na Saudi Arabia na limekuwa likipigana katika maeneo ya karibu na mji huo mkuu wa Syria.
Majuzi lilijiunga na makundi mengine ya upinzani mjini Riyadh katika kuunda mkakati wa kufanikisha mazungumzo ya amani na serikali.
Hayo yakijiri, mabasi kadhaa yamewasili katika kambi ya wakimbizi ya Yarmouk nchini Syria, kabla ya kuanza rasmi wakati kuwaondosha wapiganaji waasi, wakiwemo wanachama wa kundi la wanamgambo wa Islamic State na familia zao.
Muda huo, ulifanikishwa na Umoja wa Mataifa ungali kufahamika, lakini runinga ya Hezbollah na kundi la kutetea haki za kibinadamu la Syrian Observatory, linasema kwamba mabasi 18 tayari yamefika huko kuwahamisha waasi hao kutoka katika kambi zao zilizozingirwa kusini mwa mji wa Damascus.
Watapewa ulinzi maalum, hadi waingie salama katika kambi yao kuu, iliyoko katika mji wa Raqqa.

by Nickson John

Raia wa Rwanda wanaoishi nje ya nchi wanapiga kura ya maoni ya marekebisho ya katiba, ambayo yakiidhinishwa yatamruhusu Rais Paul Kagame kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Raia wanapigia kura katika afisi za ubalozi.
Mabadiliko hayo yakiidhinishwa, huenda yakamuwezesha Bw Kagame kusalia madarakani hadi 2034.
Raia walioko Rwanda watapiga kura hapo kesho Desemba 18.
Marekani imetoa wito kwa Bw Kagame kuonyesha uzalendo na kuondoka madarakani muda wake ukimalizika mwaka 2017.
Lakini kiongozi huyo ayashambulia mataifa yanayotoa wito huo, akisema yanaingilia maswala ya ndani ya taifa hilo la Afrika Mashariki.
Mwezi uliopita, Bunge la Seneti nchini Rwanda liliidhinisha marekebisho hayo na kupisha kuandaliwa kwa kura ya maoni.
Bw Kagame atakuwa radhi kuwania urais kwa muhula mwingine wa miaka 2017 marekebisho yakiidhinishwa.
Hata ingawa marekebisho hayo yanapunguza muda wa muhula wa rais kutoka miaka saba hadi miaka mitano, na kudumisha muda wa mihula miwili, sheria hiyo haitaanza kutekelezwa hadi mwaka 2024.
Hii ina maana Bw Kagame atakuwa huru kuwania urais kwa mihula mingine miwili ya miaka mitano mitano.
Uwezekano wa marekebisho hayo kuidhinishwa katika kura ya maoni ni mkubwa, kwa mjibu wa shirika la habari la AFP.
Chama cha Kagame cha Rwanda Patriotic Front, kundi la waasi wa kabila la Tutsi, kilisaidia kukomesha mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyotekelezwa na Wahutu wenye msimamo kali.
Zaidi ya watu 800,000 - wengi wao Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa kadiri waliuawa.
Bw Kagame bado hajatangaza iwapo atawania kiti cha urais mnamo mwaka 2017 iwapo atakubaliwa kufanya hivyo.
Anatarajiwa kufanya uamuzi huo baada ya kufanyika kwa kura ya maamuzi, kwa mujibu wa gazeti la Rwanda la New Times.

posted by nick j

Maelfu ya watu wameandamana katika miji mikuu ya Afrika Kusini wakitaka kutimuliwa kwa Rais Jacob Zuma.
Wanasema visa vya ufisadi na mapendeleo vimeongezeka sana.
Makundi yaliyoandaa maandamano hayo yamekuwa yakitumia kitambulisha mada #zumamustfall kutafuta uungwaji mkono mtandaoni.
Maandamano hayo yamefanyika Siku ya Maridhiano, siku ya mapumziko ambayo lengo lake ni kuleta pamoja watu wa asili mbalimbali Afrika Kusini.
Mwandishi wa BBC Karen Allen aliye nchini humo anasema amekutana na mmoja wa walioshiriki maandamano dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi 1976.
Anasema maandamano hayo ni kama “mwanzo wa jambo”.
Amesema hiyo ni mara yake ya kwanza kushiriki maandamano tangu wakati huo.
Bintiye mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nodel Askofu Desmond Tutu naye amejiunga na wanaomtaka Rais Jacob Zuma ang’atuke.
Amenukuliwa na tovuti ya habari la DispatchLive akisema: "Huwa twawachagua viongozi wetu na tunaweza kuwang’atua.”
Mpho Tutu ameambia mkutano mkubwa wa #ZumaMustFall mjini Cape Town kwamba wanataka ufisadi nchini humo ukomeshwe.
Wakosoaji wa Rais Zuma wanasema ufisadi umezidi chini ya utawala wake.
Amekanusha vikali madai hayo.
Leo Bw Zuma, akiongoza sherehe za kuadhimisha Siku ya Maridhiano, ameahidi kukabiliana na ukosefu wa usawa miongoni mwa watu wa asili mbalimbali.
Hakuzungumzia maandamano dhidi yake.

posted by nick j

Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.
Dar es Salaam.
Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ametoa siku 14 kwa maofisa kazi wote nchini, kukagua mikataba ya ajira kama inaendana na kanuni na sheria za ajira nchini.
Mhagama alitoa agizo hilo jana jijini Dar es Salaam, alipotembelea kiwanda cha kutengeneza nguo cha Tooku Tanzania Germent kilichopo Mabibo External, ambacho wafanyakazi wake waligoma Jumatatu ya wiki hii wakiomba kuongezwa mishahara .
Akiwa ameongozana na Naibu wake, Antony Mavunde, na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage aliwataka maofisa kazi kumpa mrejesho baada ya siku 14, huku akitaka uongozi wa kiwanda hicho kumpa majibu ya malalamiko ya wafanyakazi hao ndani ya saa nane.
“Jambo hili halikubaliki wakati kuna maofisa kazi wameajiriwa kwa ajili ya kazi hii. “Naomba mnipe maelezo ya kutosha baada ya siku hizo 14 na uongozi wa kiwanda hiki, nawapa saa nane hadi kufika saa 10:00 jioni(jana) muwe mmenipa majibu sahihi kama mtawaongezea mishahara au mnafunga kiwanda,” alisema.
Awali, Mhagama alikutana na wafanyakazi wa kiwanda hicho na kuwataka kuendelea na shughuli zao wakati wakitafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hilo.
“Waziri ametuomba tuendelee na kazi suala letu litatatuliwa, tumekubali kuendelea na kazi tukisubiri majibu ya waziri na uongozi ili tujue mwisho wetu nini,” alisema Faith Ruben mmoja wa wafanyakazi kiwandani hapo.

posted by nick j

Bado Rais Magufuli anaendelea kuipanga Serikali ya awamu ya tano ili kuhakikisha mambo yanakuwa sawa kwenye utawala wake na kazi inakwenda. Tuhuma za rushwa na ubadhirifu zimekuwa nyingi, baada ya ishu ya makontena bandarini, ukwepaji kodi TRA, kaigeukia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU.
Rais Magufuli amefanya mabadiliko Taasisi ya TAKUKURU na kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dk. Edward Hoseah ambapo kamteua aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Valentino Mlowola kukaimu nafasi hiyo.
posted by nick j

Waislamu wa dhehebu ya Shia kaskazini mwa Nigeria wameandamana kupinga operesheni wa kijeshi ambayo wanasema ilisababisha vifo vya mamia ya waumini.
Maandamano yalishuhudiwa katika miji sita mita mikuu, mji wa Kaduna ukiathirika zaidi.
Rais wa Iran, Hassan Rouhani alimpigia simu mwenzake wa Nigeria Muhammadu Buhari kuhusu operesheni hiyo ya jeshi.
Iran ni taifa la Kishia.
Jeshi la Nigeria linatuhumu dhehebu hilo la Kishia kwa kujaribu kumuua mkuu wa jeshi Jenerali Tukur Buratai.
Dhehebu hilo kwa jina Islamic Movement of Nigeria (IMN), limekanusha madai hayo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran, kwenye mawasiliano yake na Bw Buhari, Bw Rouhani aliuliza kuhusu hatima ya Sheikh Ibraheem Zakzaky, kiongozi wa IMN aiyekamatwa baada ya wanajeshi kuzingira nyumba yake katika mji wa Zaria.
Dhehebu la IMN linasema mamia ya waumini wake waliuawa na wanajeshi na madhabahu ya kundi hilo yakaharibiwa kwenye operesheni ya kijeshi.
Mtetezi wa haki za kibinadamu Chidi Odinkalu, ameunga mkono takwimu zinazotolewa na kundi hilo na kumtaka Rais President Buhari kuunda tume huru ya uchunguzi
“Haiwezekani. Wanigeria wana haki ya kuishi. Jeshi linawezaje kukabili watu wanaoandamana wakirusha mawe kwa bunduki?” Bw Odinkalu ameongeza.
Kundi la IMN lina makao makuu yake IMN na wafuasi wa dhehebu hilo waliandamana, huku vikosi vya usalama vikishika doria.
Mwandishi wa BBC Nura Muhammed Ringim anasema watu wengi walisalia manyumbani wakihofia usalama.
Miji ya Kano, Katsina, Sokoto, Zamfara na Bauchi pia ilishuhudia maandamano.
Nchini Iran, kundi la watu lilikusanyika nje ya afisi za Umoja wa Mataifa mjini Mashhad kupinga maandamano hayo, kwa mujibu wa shirika la habari la kibinafsi la Tehran Tasnim.
Jeshi halijatoa idadi ya watu waliofariki, lakini limekanusha madai kwamba mkewe kiongozi huyo wa IMN Zeenat Ibrahim aliuawa.
Meja Jenerali Oyebado, mkuu wa jeshi wa Kaduna, alisema Jumatatu kwamba mwanamke huyo anazuiliwa na jeshi.
Hakuthibitisha wala kukana madai ya kuuawa kwa mwana wa kiume wa Sheikh Ibraheem Zakzaky, Sayyid Ibraheem Zakzaky.
Mwaka uliopita, wana watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky waliuawa kwenye makabiliano kati ya jeshi na wafuasi wa dhehebu hilo.

Mahakama ya juu zaidi Korea Kaskazini imemhukumu mhubiri kutoka Canada kifungo cha maisha jela na kazi ngumu.
Hyeon Soo Lim, 60, aliyekamatwa mjini Pyongyang baada ya kuzuru taifa hilo Januari kwa kazi ya kibinadamu amehukumiwa kwa makosa ya “uhalifu dhidi ya dola.”
Bw Lim, ambaye ni kiongozi wa Light Korean Presbyterian Church, alikuwa ameenda kusaidia kituo cha kutunza wagonjwa, kituo cha kuwatunza watoto na kituo cha kutunza mayatima.
Mhubiri huyo kutoka Korea, anadaiwa kukiri kuhusika katika njama ya kupanga kupindua serikali na kuunda taifa la kidini.
Shughuli zozote za kidini ni marufuku nchini Korea Kaskazini.
Taifa hilo mara kwa mara huwakamata na kuwazuia wageni wanaoenda huko kwa shughuli za kidini au kimishenari.
Bw Lim alihukumiwa baada ya kesi yake kuendeshwa kwa muda mfupi na mahakama ya juu ya Korea Kaskazini.
Inadaiwa mhubiri huyo amekiri kutoa mihadhara na kusema “Korea Kaskazini inafaa kusambaratishwa na mapenzi ya Mungu”, na kusaidia Marekani na Korea Kusini kutoa usaidizi kwa wanaotoroka Korea Kaskazini.

 Kumekuwa na ripoti mfululizo kuhusu ishu ya hali mbaya ya hewa iliyokumba nchi ya China ikafikia hatua mpaka baadhi ya viwanda vikalazimika kufungwa kwa muda.
December 14 2015 nilikusogezea ripoti ya mgahawa mmoja China kuwatoza wateja wote kama Yuan 1 ambazo ni kama Tshs. 333 hivi kwa ajili ya kupata hewa safi ndani ya mgahawa huo,
Leo nimeinasa ripoti CNN kwamba kuna kampuni moja ya Vitality Air ya Canada imeamua kutengeneza chupa zilizojazwa hewa safi ambazo zinasafirishwa na kwenda kuuzwa China.
Gharama ya chupa au kopo moja la hewa ni kati ya dola 14 mpaka 20 ikitegemeana na ujazo wa kopo lenyewe !!
posted by nick j von luvendowski



 
Meli ya mizigo katika bandari ya Mombasa walipokamatwa wavuvi wa Pemba.
Meli ya mizigo katika bandari ya Mombasa walipokamatwa wavuvi wa Pemba.



Maafisa wa usalama wa Kenya wanasema wamekamilisa kuwakagua watu zaidi ya 100 waliokamatwa mwishoni mwa juma kwenye bahari hindi, na imetambua kwamba walikuwa ni raia wa Tanzania pamoja na wakenya kadhaa.
Wakuu wa Usalama kutoka eneo hilo wamesema japo wengi wao ni wavuvi kutoka Pemba, waliokuwa wakivua nyakati za usiku, watafunguliwa mashitaka ya kuingia nchini kinyume cha sheria na kuchukuliwa kama wahamiaji wasio na hati zinaozhitajika.
Watu hao wote ambao ni wanaume walikamatwa kwa sababu za kiusalama kulingana na mkuu wa idara ya polisi katika county ya  Mombasa, Francis Wanjohi ambae pia amesema kuwa uchunguzi uaonyesha kuwa walikuwa wavuvi. Hata hivyo amesema idara ya uhamiaji na ile ya uvuvi zitachukua hatua za kisheria dhidi ya washukiwa hao.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget