Halloween Costume ideas 2015
Articles by "KENYA"

Chuo kikuu cha Garissa kilichofungwa mwaka uliopita baada ya watu 148 kuuawa kwenye shambulio lililotekelezwa na wanamgambo wa al-Shabab, kimefunguliwa tena.
Wafanyakazi wamefika kazini leo huku usalama ukiwa umeimarishwa.
Kila aliyekuwa akiingia katika chuo kikuu hicho kilichoko eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya amepekuliwa na maafisa wa usalama.
Kituo cha polisi, ambacho kitakuwa na maafisa zaidi ya 20 wa kutoa ulinzi, kimejengwa ndani ya chuo kikuu hicho.
Kitambulisha mada #GarissaUniversityReopens (Chuo Kikuu cha Garissa chafunguliwa tena) kimekuwa kikivuma katika mtandao wa Twitter nchini Kenya.
Wengi wanasema kufunguliwa kwa chuo hicho kunaonyesha Wakenya hawawezi kuvunjwa moyo na magaidi.
Msimamizi mkuu wa chuo kikuu hicho Prof Ahmed Warfa ameambia BBC kwamba wanafunzi wataanza kufika chuoni Jumatatu ijayo tarehe 11 Januari.
Hakukukuwa na sherehe yoyote maalum ya kuadhimisha kufunguliwa upya kwa chuo hicho.
Wengi wa wanafunzi wanaofadhiliwa na serikali walionusurika shambulio hilo la mwezi Aprili walihamishiwa Chuo KIkuu cha Moi, Eldoret.
Wanafunzi wa kujitegemea ndio wanaotarajiwa kurejelea masomo Jumatatu.
Mwandishi wa BBC Bashkas Jugsodaay anasema kufunguliwa kwa chuo kukuu cha Garissa ni afueni kwa wakazi na viongozi wa mkoa wa Kaskazini Mashariki ambao wamekuwa wakiisihi serikali kufungua chuo hicho, kwa walikuwa wakikitegemea kwa ajira na wateja. Wengi walikuwa wakinufaika
Wanafunzi zaidi ya 800 walikuwa wakisomea taaluma mbalimbali katika chuo hicho kabla ya kushambuliwa na magaidi Aprili mwaka jana.



 

Ikiwa Mwezi Novemba mwaka uliopita wapiganaji wa Al Shabaab waliteka basi moja na kuwaua abiria 28 ambao hawakuwa Waislamu bado kundi hilo liligonga vichwa vya habari mwezi Aprili lilipowaua wanafunzi wakristo 148 katika chuo kikuu cha Garissa.

 Imeripotiwa tena watu wawili wameuwawa na wengine watatu kujeruhiwa vibaya baada ya wapiganaji wa kundi la al Shabaab kushambulia basi moja la abiria lilokuwa likielekea eneo la Mandera Kaskazini mwa kenya kutoka Nairobi.

Shambulio hilo la kigaidi lilitekelezwa hii leo asubuhi.
Walioshuhudia wameweka bayana kuwa raia wa  kiislamu waliwalinda wenzao wakristo kwa kukataa kugawanywa kwa makundi.

Wasafiri waislamu nchini Kenya walilazimika kuingilia kati kuokoa maisha ya wakristu waliokuwa nao katika basi lililotekwa na wapiganaji wa Alshabaab.
Waislamu hao walitahamaki walipotekwa na wapiganaji wa Al Shabaab kisha wakaanza kutenganishwa katika makundi mawili ya waislamu na wasio waislamu.

Hapo ndipo waligundua nia yao ni kuwaua kama walivyofanya katika mauaji kama hayo mwaka uliopita.
Mhudumu wa kampuni ya basi la Makkah ameithibitishia kutokea kwa tukio hilo katika barabara ya kutoka Mandera kuelekea mjini Nairobi.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget