Halloween Costume ideas 2015
Articles by "DAR ES SALAAM"

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Sifuni Mchome.


SHULE nyingi za msingi na sekondari zisizo za Serikali, zimetuma maombi kwa Kamishna Mkuu wa Elimu nchini kuomba kibali cha kupandisha ada katika mwaka ujao wa masomo.

Hatua hiyo ni kuitikia amri ya Serikali ya kuzipiga marufuku shule binafsi, kupandisha ada kiholela na badala yake shule zote zinatakiwa kuwasilisha maombi ya kupandisha ada hiyo mpya kwa kamishna huyo ili yajadiliwe.
“Kwa kweli baada ya tangazo lile shule nyingi zimeleta maombi yao hapa na kilichobaki ni kwa kamishna wa elimu kuhakikisha anapitia maombi hayo kwa kuzingatia vigezo mbalimbali vilivyowekwa na Serikali,” alisema Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Sifuni Mchome.

Alisema lengo la maombi hayo ni kuondoa tabia ya wamiliki wa shule zisizo za Serikali, kupandisha ovyo ada kwa kadiri wanavyotaka, jambo lililosababisha shule nyingine kugeuza elimu kuwa biashara badala ya kutoa huduma.

Lengo la wizara hiyo ya kutaka maombi hayo na kiwango cha ada wanazotoza kwa sasa ni kubaini shule, ambazo zinafanya biashara na zile ambazo zinatoa huduma ya elimu kwa kuisaidia Serikali. Shule ambazo zitabainika kufanya biashara, zitatakiwa kulipa kodi kutokana na biashara hiyo wanayoifanya.
Profesa Mchome aliwataka wazazi kuisaidia Serikali kwa shule ambazo hazitafuata utaratibu huo, watoe taarifa kwa halmashauri za wilaya, wizarani ili kuhakikisha zile ambazo zimekaidi agizo hilo, zinachukuliwa hatua.
“Hizi shule ni nyingi ziko zaidi ya 1,000, naomba wazazi watusaidie kwa shule ambazo zitakaidi agizo la Serikali watuletee taarifa ili tuweze kuchukua hatua kwa shule husika,” alisema Profesa Mchome ambaye alisisitiza kuwa wazazi wafanye vikao na shule husika kuhusu upandishwaji ambao unatangazwa na shule husika.

 
Serikali imesitisha zoezi la bomoabomoa kwa muda wa siku 14 ili kuwapa muda wa kutosha watu waliovamia na kuishi katika bonde la Mto Msimbazi Mkwajuni kuondoka, ambapo imesisitiza kuwa baada ya siku hizo kuisha zoezi hilo litaanza tena na hivyo wahakikishe wanaondoka  wenyewe.

Akitoa tamko hilo waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh William Lukuvi amesema waliojenga katika eneo hilo wapo hapo  kinyume na sheria  kwa sabubu ni mahali hatarishi.
 Akaongeza kuwa kuanzia mwakani wizara yake itagawa kwa viongozi wa serikali za mitaa ramani za mipango miji ili waweze kuzisimamia kwa ukaribu ili kuepusha uwezekano wa kutokea ama kufanya ujezi holela.
 
Aidha baadhi ya wananchi wamepongeza zoezi za bomoabomoa na kusema kuwa imekuwa na hatua ngumu lakini muhimu kwani eneo hilo limekuwa likisababisha vifo vya watu kila mafuriko yanapotokea hivyo watu kuondolewa hapo wamenusurishwa kwa mengi.
 
Katika hatua nyingine waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Mh Jenister Mhagama ameziagiza kamati za maafa katika ngazi za mikoa, wilaya na vijiji kuorodhesha na kuwapa barua za kuwataka watu wote wanaoishi maeneo hatarishi kuhama mara moja katika maeneo hayo na utekelezaji wa agizo hilo uwasilishwe ofisi ya waziri mkuu haraka iwezekanavyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Ndugu Reverien Ndikuriyo Spika wa Seneti na Mjumbe Maalum wa Rais wa Burundi


RAIS John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Seneti na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Burundi, Reverien Ndikuriyo Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu hali ya kisiasa na usalama nchini Burundi na jitihada zinazochukuliwa na Tanzania, ikiwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Akiwasilisha ujumbe wa Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi kuhusu hali ya Burundi, Spika Ndikuriyo alisema Serikali ya Burundi ipo tayari kufanya mazungumzo na wadau wote wa siasa kuhusu hali ya nchi hiyo na jitihada za kuumaliza mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

Akitoa maelezo ya kikao hicho kwa niaba ya Dk Magufuli, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk Augustine Mahiga alisema Serikali ya Burundi imekubali usuluhishi, unaofanywa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa niaba ya Marais wa EAC kutokana na kikao kilichofanyika Dar es Salaam Julai mwaka huu na kwamba Serikali ya Burundi iko tayari kushiriki mazungumzo hayo ya amani.
“Nimeagizwa nipeleke taarifa kwa mawaziri wa nchi za nje wa nchi jirani juu ya maandalizi ya mazungumzo hayo ambayo yataanza kule Uganda tarehe 28 mwezi Desemba”, alisema








RAIS wa awamu ya tano Dk. John  Magufuli,  ametoa zawadi  ya vyakula, mbuzi na mafuta ya kupikia zenye  thamani   ya Sh  mil  8,089, 000  kwa watu walio katika makundi  maalum wakiwemo watoto wanaoishi katika  mazingira hatarishi,watu wenye ulemavu pamoja na wazee.

Akikabidhi msaada huo katika kituo cha kulelea watoto wanaokinzana na sheria kilichopo Upanga jijini Dar es Salaam, kwa niaba ya Dk. Magufuli, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Rabikira  Mushi,  alisema katika kusheherekea sikukuu za maulid,Chrismas  na mwaka mpya Dk Magufuli ameamua kutoa zawadi katika vituo nane  katika mkoa wa Dar es Salaam , viwili  Zanzibar na Vituo Vitano toka mikoani kwa Tanzania Bara.

Alitaja vituo hivyo kuwa ni  Makao ya Taifa ya watoto yatima Kurasini,mahabusi ya watoto Upanga kilichopo Ilala,Makao ya Wazee na wasiojiweza  Nunge Kigamboni,Chuo  cha Ufundi kwa watu wenye ulemavu Yombo, Kituo cha Mother Theresa  Mburahati  Kinondoni,Kijiji cha Furaha Mbweni kilichopo Kinondoni, Dar al arqum Tandika (Temeke) na kituo cha watoto Msimbazi, Kwa Zanzibar  kituo cha Maboani Chakechake Pemba  na Cha wezero Unguja.

Alisema kwa mikoa ya Tanzania  Bara  vituo vilivyopatiwa msaada ni Makao ya watoto Kemondo(Bukoba), Kituo cha Village of Hope(Dodoma),Shule ya maadirisho Irambo(Mbeya), Makazi ya wazee wasiojiweza Bukumbi,Misungwi(Mwanza) na Makazi ya wazee wasiojiweza Sukamahela, Manyoni, (Singida).
“Lengo la Dk. Magufuli  kutoa zawadi hiyo ni kuwawezesha makundi hayo   ya weze kusheherekea  sikukuu kama ilivyo kwa watu wengine.”alisema Mushi.

Meneja wa mahabusu ya watoto Upanga, Ramadhani Yahaya alisema wanamshukuru rais Dk. Magufuli kwa ukarimu wake hasa kuwakumbuka watoto wa ukinzani wa sheria na kudai kuwa mara nyingi wadau  wamekuwa hawawakumbuki.
“Tunawaomba wadau wengine wawe na moyo wa kuwasaidia watoto hawa, pia tuna matatizo ya ufinyu wa bajeti katika serikali kunahuduma muhimu ambazo tunazikosa  tunaomba wadau mbalimbali wajaribu kusaidia kutujengea uzio  kwakuwa serikali itachukua muda kutatua tatizo hilo”.alisema Mushi.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe MAgufuli
 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkesha mkubwa wa kuiombea amani  Tanzania  utakaofanyika Disemba 31 mwaka huu katika uwanja wa Taifa.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Pentekoste (TFC)    Godfrey Malassy alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijin Dar es Salaam, na kuthibitisha  kuwa maandalizi yote yamekamilika ikiwemo kibali kutoka polisi, pamoja  washiriki mbalimbali watakaoshiriki katika mkesha huo.
 
Askofu Malassy ameongeza kuwa mkesha huo  utakuwa ni kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kuijalia nchi yetu kumaliza Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu kwa amani na utulivu,pamoja na Dua maalum ya kumuombea Mhe. Rais afya njema na utendaji mzuri anaoendelea kuufanya kwa maendeleo ya Taifa letu kwa kuwa mara zote amesisitiza kufanyiwa maombi na watanzania.
“Tutatumia nafasi hiyo kumuombea Mhe.Rais katika kutekeleza jukumu kubwa alilokabidhiwa na  watanzania kuongoza Taifa letu ili aweze kufanikiwa katika hilo.”Alisema Askofu Malassy.
 
Aidha Mwenyekiti huyo amewataka wananchi wote kutumia siku hiyo kumuomba na kumshukuru Mungu kwa amani iliyopo nchini kwa vile ndio msingi mkubwa wa shughuli za kila siku zinazosaidia kupata kipato na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Naye Mch.Olivia Mallonga ambaye ni mjumbe katika kamati ya maandalizi ya Mkesha huo amesema kwamba wao kama wadau   wanaendeleza desturi ya kuliombea Taifa amani ili lisije kutumbukia kwenye machafuko kama nchi nyingine .
 “Watanzania wana dini ndio maana wanatumia  imani zao kufanya maombi ili Mungu awalinde na maovu au machafuko yanayoweza kutokea kutokana na sababu yoyote.”Aliongeza Mch. Olivia. Mkesha huo ni wa 17 tangu ulipoanza kufanyika Tanzania na umeleta mafanikio makubwa ikiwemo kuunganisha watanzania bila kujali imani  zao.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema hana orodha ya majina ya watu wanaouza dawa za kulevya na hana muda wa kushughulika na hiyo inayoitwa orodha.

Badala yake, amesema chini ya uongozi wake ataweka mifumo itakayosaidia kudhibiti uingizaji wa dawa hizo nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kufanya kikao na maofisa wa ngazi ya juu wa Polisi, Kitwanga alisema wamekubaliana kuhakikisha dawa za kuleya zilizoko nchini zinakamatwa na kuteketezwa.

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mh. Charles Kitwanga.   (Picha kutoka Maktaba)

“Mimi hapa nilipo sina orodha ya wauza dawa za kulevya na wala Rais hajanipatia hiyo orodha na siamini kama Rais anayo…ila ninachowaambia ni kwamba tumekubaliana kuweka mifumo mizuri ya kuwakamata watu wote ambao watakutwa na dawa hizo,” alisema Kitwanga.

Alisema mifumo hiyo haitajali ukubwa na nafasi ya mtu kwenye jamii.Maana mifumo hii tunayoiweka haijali vigogo wala sisimizi na nawahakikishia kwamba tumejipanga kumaliza tatizo hili la dawa za kuleya,” alisema.

Alisema katika kikao hicho wamekubaliana kuongeza nguvu kuhakikisha wanawakamata watu wote ambao wanahusika na biashara haramu ya kuingiza dawa za kulevya na kuzisambaza nchini.

Akizungumza kutokuwepo kwa polisi katika Bandari ya Dar es Salaam, alisema wanaendelea kufanya mazungumzo na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kuona utaratibu mzuri wa kupeleka ulinzi kwenye eneo hilo ili kuweza kudhibiti utoroshaji wa vitu mbalimbali ambavyo vinatoka bila utaratibu.

Katika hatua nyingine, Kitwanga aliwataka polisi kuwashitaki watu kwa kesi walizo nazo na sio kuwabambika  kesi watu wasio na hatia na  kusababisha kufungwa kwa kesi zisizowahusu.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget