Kampuni kubwa ya Bia nchini Tanzania (TBL) imefanikiwa kuwa muajiri bora kwa mwaka 2015,katika Tuzo za kila mwaka zitolewazo na na shirikisho la Waajiri Nchini (ATE)
Tuzo hizo zilizofanyika katika Ukumbi wa Mlimani city na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa, TBL pia iliibuka mshindi katika vipengele vya Uongozi na usimamizi bora,Utawala na usimamizi wa Rasilimali watu,Ubora na uzalishaji,ushirikishaji wa wenye ulemavu na kampuni bora kubwa.
Post a Comment